Nyingine

Orodha ya washindi wa tuzo za EATV zilizotolewa usiku Desemba 10

Leo Desemba 10, 2016 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam zimetolewa tuzo kwa wasanii mbalimbali wa muziki na wa filamu kutoka nje na ndani ya Tanzania.

Jumla ya tuzi 9 zilizotelewa kwa wasanii mbalimbali waliofanya vizuri kwa mwaka 2016 ambapo tuzo moja ya heshima ilitolewa kwa mtu aliyekuwa na mchango mkubwa katika saanaa ya Tanzania na hivyo kufanya jumla ya tuzo 10. Tuzo hii ilitolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.

Hapa chini ni orodha ya washindi wa tuzo mbalimbali zilizotolewa usiku wa Desemba 10.

1. Tuzo ya Filamu Bora ya Mwaka- Safari ya Gwalu
2. Wimbo Bora wa Mwaka- Aje wa Ali Kiba
3. Video Bora ya Mwaka- Aje ya Ali Kiba
4. Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kiume- Salim Ahmed maarufu Gabo
5. Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kike-  Chuchu Hans
6. Kundi Bora la Muziki- Navy Kenzo
7. Mwanamuziki Bora Chipukizi- Amani Khamis maarufu Man Fongo
8. Tuzo ya Heshima- Dj Bonny Love
9. Mwanamuziki Bora wa Kike- Judith Wambura maarufu Lady JayDee
10. Mwanamuziki Bora wa Kiume- Ali Kiba

Mwanamuziki Ali Kiba ameweka rekodi katika tuzo hizi zilizotolewa kwa mara ya kwanza baada ya kutwaa tuzo tatu ikiwa ni Video Bora ya Mwaka, Wimbo Bora wa Mwaka, na Msanii Bora wa Kiume.

Soma na hizi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close