Sambaza:

Napenda sana Opera browsers. Kampuni hii ni taasisi ambayo imetengeneza na kutoa browsers kwajili ya vifaa mbalimbali, browsers zenye ubora na zinazoshindana vizuri kwenye soko. Hivi sasa, natumia toleo jipya la Opera browser na inaubora zaidi kuliko Chrome katika baadhi ya matukio, lakini kwa simu ni hadithi nyingine.

Opera imekuwa ikihodhi soko la browser za simu kwa muda mrefu sasa nani kutokana na sifa yake ya kuokoa data ambayo inapatikana kwenye apps zake kama Opera Mini. Inapatikana kwajili ya Android, iOS na Windows Phone na inatumiwa na watu ambao wanafahamu matumizi yao ya data.

SOMA NA HII:  Simu Bora Zenye Kamera Nzuri Mwaka 2018

Sasa betanews waliwasiliana na Opera kuhusu hali ya maendeleo ya browser yao kwajili ya iOS na wao wametoa jibu la kushangaza kama inavyoonekana kwenye tweet hapa chini:

Mwandishi aligundua kwamba Opera browsers kwajili ya iOS haijafanyiwa maboresho tangu mwaka 2017 uanze, ambapo ni jambo lisiyo la kawaida. Alipoiuliza kampuni hiyo kwa nini wamefanya hivyo, msemaji wa Opera anayefahamika kwa jina la Rosi alibaini kuwa kampuni haina timu ya watu wanaofanya kazi kwajili ya iOS na ndiyo maana kulikuwa hakuna maboresho.

Opera Coast for iOS mala ya mwisho kufanyiwa “update” ilikuwa Desemba mwaka jana, ambapo ni miezi 6 iliyopita na Opera Mini ndio ipo kwenye hali mbaya zaidi(Miezi 11 iliyopita). Hii ina maanisha kuwa watumiaji wa iOS wanatakiwa kutumia browser za nje wanatakiwa kutumia Firefox ama Chrome kama hawapendi kutumia Safari.

SOMA NA HII:  Simu za zamani zilizovuma miaka ya 2000 - 2005

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako