Kila mtengenezaji wa simu amekutana na matatizo ya jinsi ya kusambaza matangazo kwa watumiaji wake. Hii imetokea karibuni kwa kampuni ya HTC ambayo imekutana na tatizo la matangazo kuonekana kwenye keyboard yake. Kawaida ni tatizo na limerekebishwa. OnePlus kwa upande mwingine wanafanya hivyo kwa makusudi.

Simu ya OnePlus

Watumiaji wengine wa OnePlus wanaripoti kwamba wanapata taarifa za kushinikiza (push notifications) kwajili ya utafiti ili kushinda OnePlus 5. Mwanzo, taarifa za kushinikiza zilikuwa zinatangaza uzinduzi wa kifaa kipya.

Matangazo haya yanasambazwa na app ya mfumo wa kampuni yenyewe, kitu ambacho sio kizuri kwa wateja wake. Kivuli cha taarifa ni eneo takatifu kwa watumiaji wa Android, hivyo ni bora matangazo yaendelee kusambazwa kwa mfumo wa barua pepe.

SOMA NA HII:  Uchambuzi wa simu ya Infinix Hot S X521 na Bei yake nchini Tanzania

Chanzo: Reddit@ITheBK

Sambaza:

Written by Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako