Apps za SimuSimu za Mkononi

NQ Vault App Bora Kwa Ajili Ya Kuficha Sms, Calls, Picha na Video zako!

Simu zimekuwa kitu muhimu kwenye maisha yetu ya kila siku, kukua kwa teknolojia ya simu kumefanya simu kuwa kama kiungo mojawapo cha mwili.

Hivi sasa watumiaji wengi wa simu janja (smartphones) wanapenda kushare picha na video fupi katika mitandao ya kijamii kama instagram, facebook, twitter au whatsapp. Sio jambo baya lakini vipi linapokuja suala la uhifadhi wa picha hizi,  hasa zile tunazopenda kupiga tukiwa maeneo ya faragha au baadhi ya picha ambazo hatupendi wengine wazione?

Kuna umuhimu wa kuwa na app ya ulinzi na usalama wa picha zetu. Kuna app nyingi kwajili ya Adroid na iOS zinazofanya kazi ya kuhifadhi na kutunza picha na video za siri. Nyingi ni nzuri lakini hazikidhi moja kwa moja mahitaji ya mtumiaji wa kawaida wa simu.

Hapa ndipo NQ Vault inapoingia, Vaulty ni app bora kabisa kwa watumiaji wa simu za android na iOS. Vault kutoka kwa NQ Vault ina uwezo mkubwa sana linapokuja suala la utunzaji wa data zako za siri.

Baadhi ya Faida za NQ Vault ni:

  • Kuficha picha na video na kuzifanya zisionekane hata kwa kuchomeka simu kwenye kompyuta
  • Kuficha sms na missed calls za baadhi ya namba ulizozichangua.
  • Ku-backup picha na taarifa zako za siri mtandaoni kulingana na uhitaki wako.
  • Uwezo wa kuficha icon ya app yenyewe
  • Uwezo wa kulock app muhimu.
SOMA NA HII:  Simu za zamani zilizovuma miaka ya 2000 - 2005

Hizo ni baadhi ya vitu unavyoweza kufaidika navyo kwa kutumia app hii.

Kama wewe ni mtumiaji wa Adroid ama iOS unaweza kupakua App ya NQ Vault  ili kuficha SMS, Picha, Video na kufunga Apps muhimu kwenye simu yako.

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa Mediahuru Kila Siku, Karibu Kwa Pamoja Tujenge Jamii Ya Wanateknolojia!.

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako