Kompyuta

Notebook 9 Pro Laptop Ya Kwanza Kutoka Samsung Inayokuja na S-Pen.

Jana, Samsung walizindua “Notebook 9 Pro” komputa ndogo ikiwa na Windows 10. Ni ajabu, licha ya kuwa na lebo “Pro”, “laptop” hii inatumia “Windows 10 Home” tu.

Mimi nilitarajia itakuwa na Windows 10 Pro.

Moja ya vipengele muhimu ni kuingizwa kwa “S-Pen” na kama unavyoona kwenye picha hapa chini, S Pen ina hifadhiwa ndani ya kifaa, badala ya “magnetic solution” inayotumiwa na Microsoft.

Ukiuliza mimi, nadhani Napendelea mbinu ya Samsung. Pia, Samsung wanasema ina ncha ya 0.7mm na “inaweza kugundua viwango vya shinikizo zaidi ya 4,000” (labda 4096). Pia inakuja na “Air Command”, ambayo “inakuwezesha kuchukua maelezo mafupi, kurekebisha taarifa mbalimbali na kuchora.”

Laptop hii inapatikana katika screen za ukubwa wa aina mbili(13- na 15-inch), aina zote mbili zinaendeshwa na “7th-generation Intel Core i7 Processors”. Hata hivyo, yenye screen ya 15-inch inakuja na “AMD Radeon 540 GPU”. Unaweza kuona sifa zake nyingine hapa chini:

Specs Notebook 9 Pro (13-inch) Notebook 9 Pro (15-inch)
Operating System Windows 10 Home
Processor Intel® Core™ i7 Processor 7500U (2.70GHz up to 3.50GHz 4MB L3 Cache)
Display 13.3″ FHD LED Display (1920 x 1080) with Touch Screen Panel 15.0″ FHD LED Display (1920 x 1080) with Touch Screen Panel
Graphics Intel® HD Graphics 620 AMD Radeon™ 540 Graphics with 2GB GDDR5 Graphic Memory
Memory 8GB DDR4 Memory (8GB on board) 16GB DDR4 Memory (16GB on board)
Storage 256GB SSD
Wireless 802.11 ac 2×2
Bluetooth Bluetooth 4.1
Sound 1.5 W x 2 Stereo Speakers, SoundAlive™
Integrated Camera 720p HD Camera (IR Camera)
Mic Internal Dual Array Digital Music
Keyboard Island-type keyboard, backlit, click pad, stroke 1.5mm
Other Input Touchscreen, Built-in S Pen
I/O Ports 2XUSB 3.0, 1XUSB-C, HDMI, MicroSD, HP/Mic, DC-in
AC Adapter 40W AC Adapter 60W AC Adapter
Dimensions 12.21” x 8.54” x 0.63’ 13.67” x 9.41” x 0.67”
Weight 2.91lbs 3.79lbs
Battery 54Wh, Fast Charging, External Battery Charging
Color Titan Silver
Software Wi-Fi Transfer, Wi-Fi Camera, Simple Sharing, PC Message, PC Gallery, Samsung Recovery, Samsung SideSync
Energy Star Yes
SOMA NA HII:  Orodha ndefu ya njia za mkato "Keyboard Shortcuts" za Windows 10

Kwa bahati mbaya, bei zake na upatikanaji bado haujulikani kwa sasa, hivyo naliweka swala hili kwenye mawazo yangu na nitakufahamisha zitakapo tangazwa.

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

JIUNGE NA MAZUNGUMZO, TOA MAONI YAKO HAPA

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Lako