Sambaza:

Kwa mujibu wa Venture Beat, HMD (Kampuni kutoka Finland yenye haki za kipekee kwajili ya kutengeneza vifaa vya brand ya Nokia) itatangaza simu mpya tatu: smartphones mbili za Android, na simu ya kawaida. Simu mbili za android zitakuwa Nokia 5 na Nokia 3, wakati kampuni hii itatukumbusha historia  kwa kuirudisha, Nokia 3310.

Nokia 5 inatarajiwa kuwa na 5.2-inch 720p display, 2 GB ya RAM, na  kamera ya 12 MP. Itakugharimu karibu $ 200 kuinunua. Nokia 3, inatarajiwa kuuzwa karibu $ 150. Bado haijajulikana vitu vinavyopatikana kwenye Nokia 3.

Chakushangaza (au, kwa kuwa jina ni lile lile), inasemekana Nokia 3310 itakuwa  ni “toleo la kisasa”  la simu maarufu ya Nokia 3310, iliyotoka zamani sana mwaka 2000. Nokia 3310 iliuza zaidi ya simu milioni 100, ilikuwa inajulikani kwa kudumu muda mrefu sana na kuaminika, huku ikiwa na betri inayoishi muda mrefu. Hakuna taarifa kuhusu sifa za toleo la kisasa la Nokia 3310, lakini mpaka sasa inasemekana inaweza kugharimu karibu $ 60.

SOMA NA HII:  Wanafunzi wa Primary Tanga kuanza kusoma kwa kutumia Tablet

Bei hii mpya inaonekana kama ndogo , lakini naamini simu hii itawashinda wamiliki wa zamani, na kuwavutia mashabiki wa Nokia, ambao watainunua kwa ajili ya matumizi kama simu pili.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako