Simu za Mkononi

Nokia 3310 (2017) yaanza kuuzwa Afrika ya Kusini na Nigeria ila sio Tanzania

HMD Global wamethibitisha kuwa simu mpya ya Nokia 3310 itaanza kuuzwa katika nchi za Afrika ya kusin na Nigeria. Simu hii itazinduliwa Afrika ya Kusini katikati ya mwezi wa sita na itaanza kwa kuuzwa shilingi  R699 (Tsh.119265 / $53.48) na itakuwa inauzwa kupitia mtandao wa simu za mkononi MTN.

Nikukumbushe, Nokia 3310 mpya inaendesha na programu ya “Nokia Series 30+ programu, 2.4-inch QVGA polarized na kioo chenye rangi , kamera yenye 2 MP, hifadhi ya ndani yenye ukubwa wa 16MB ila unaweza kuongeza uwezo wa kuhifadhi kupitia “Micro SD card”  hadi GB 32, inatumia muunganisho wa mtandao wa 2G na kuingia kwenye mtandao kupitia Opera Mini browser na ina betri ya 200 mAh.

Nokia 3310 mpya inapatikana katika rangi nne: nyekundu, njano na bluu na kijivu.

HMD Global ilizindua toleo jipya la Nokia 3310 mwezi Februari, walisema wameichukua Nokia 3310 ya zamani na “kuiboresha katika muonekana wa 2017”.

Simu hii ilianza kuuzwa nchini Uingereza wiki iliyopita kwa bei ya £ 49.99 na mauzo yake yamekuwa mazuri.

Hata hivyo, kama wewe hujaipenda simu hii ya Nokia 3310, Caviar – wauzaji wa simu za kifahari- wametoa aina nyingine ya Nokia 3310 ambayo ina vitu vingi pia ina picha ya rais wa Urusi inauzwa $ 1690.

Hatuna taarifa kamili simu ya Nokia 3310 (2017) itauzwa shilingi ngapi nchini Nigeria ila tunajua itaanza kuuzwa nchini Nigeria.

SOMA NA HII:  Fahamu Uwezo na Bei ya simu ya Tecno L8

Kuhusu kuuzwa nchini Tanzania na Afrika ya Mashariki kwa ujumla, HMD wamesema:

“…Further announcements will be made for other key markets as it becomes available.  At this stage we’ve only confirmed South Africa and Nigeria.”

Hii ni stori ya kuvutia kuhusu simu ya zamani ya Nokia 3310:  Kwa Hiyo Ni Kweli Watu Wanatumia Simu Za Zamani Za Nokia Kama Sex Toys ?!

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako