BloguMaujanja

Njia za kupunguza Blog kuchelewa kufunguka

Muda unaotumika wakati wa kufunguka kwa blog yako “Blog loading time” ni kitu cha muhimu ambacho kila blogger anapaswa kukizingatia kwa sababu inaweza kuchangia ukapoteza watembeleaji wa blog yako.

Hakuna anayependa kusubiri kwa muda mrefu ili website yoyote ile ifunguke, Pia Google hutumia speed ya website kama njia ya kufanya site’s page rank.

Kwa hiyo leo nitaeleza jinsi ya kupunguza muda unaotumika ili website yako iweze kufunguka haraka kuongeza page ranking kwenye Google. Njia za kupunguza blog loading time Ukifata hatua hizi zitakusaidia:

1. Chagua web server: Server ni muhimili wa blog yako, kwa kujiunga na web server yenye uwezo wa kufanya blog ifunguke kwa haraka itachangia kufanikiwa kwa blog yako. Server yenye uwezo huu inatakiwa uwe na fedha kuipata ila ni bora kuliko kupoteza watembeleaji wa blog yako , Nakushauri ujiunge na kampuni yoyote kwajili ya hosting kwa mafanikio ya blog yako.

2. Punguza idadi ya plugins na widgets ulizotumia kwenye blog yako kwa sababu vitu hivi vinaleta madhara kwenye page loading time. Ukiwa na plugins nyingi inamaanisha kuna codes nyingi zinatakiwa kusomwa na server yako. Hapa jitahidi kuondoa plugin yoyote ile unayoona haina umuhimu kwenye blog yako.

3. Tumia theme rahisi “Use a simple theme” kwa sababu muda wa kufunguka kwa blog yako pia kunachangiwa na aina ya theme unayotumia. Jitahidi kutumia themes ambazo ni search engine friendly na zinazofunguka kwa haraka. Usipende kutumia themes zinazotegemea sana addons na plugins kufanya kazi.

SOMA NA HII:  WordPress vs. Blogger – Ipi ni Bora? (Faida na Hasara)

4. Punguza idadi ya picha zinazotumika kwenye blog yako kwa sababu picha zinatumia muda mwigi kufunguka. Mpangilio wa picha ni kitu muhimu kwa blogger kujifunza kwa sababu itasaidia kupunguza loading time ya blog kwa ujumla.

5. Hakikisha unaupdate blog yako kila mala, update plugins, blogger, theme bora kwasababu kufanya update kutasaidia kuondoa bugs na hii inachangia kuwa na performance nzuri.

6. Punguza idadi ya posts kwenye ukurasa wa mbele “homepage”.

7. Weka idadi ya comments katika ukurasa hii inachangia blog kufunguka kwa haraka .

8. Usiweke matangazo mengi kupita kiasi kwa sababu itachukua muda mwingi kuprocess ads scripts.

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.