Njia nyepesi za kubet na kufanikiwa katika Betting


Machoni mwa watu wengi, mchezo wa kubashiri matokeo (betting) huchukuliwa kama ni mchezo usiofaa katika jamii, lakini mimi naona inategemeana na wewe mchezaji unavyouchukulia na namna unavyoshiriki kuucheza.

Betting haihusishi mpira wa miguu tu kuna michezo mingine kama cricket, basketball, ngumi na nk. Huu mchezo ukiucheza kwa makini ni mchezo unaoweza kuwa msaada katika maisha yako hasa kukusaidia kuinua kipato chako.

Tuangangalie baadhi ya njia na hatua za kufuata ili kuweza kufanikiwa katika betting:

  • Sio chanzo kikuu cha mapato

Usiufanye huu mchezo wa kubet kama chanzo chako kikuu cha mapato cha kutegemea. Hii itakuepusha wewe kutoshusha kipato chako hata iwapo hutapata matokeo uliyotarajia katika betting.

  • Usitumie fedha zako muhimu

Kamwe usipende kutumia fedha zako za mambo ya muhimu katika mchezo huu (mfano fedha za kuendesha maisha yako na familia kila siku). Tumia fedha za ziada unazozipata. Hii itakusaidia wewe kuendelea na maisha yako kama kawaida endapo mambo yataenda ndivyo sivyo katika betting.

  • Zijue timu unazozibetia/ ambazo unazitabiria

Jaribu kufuatilia kwa ukaribu michezo unayopenda kubashiri, hii itakusaidia kupunguza uwezekano wa kupoteza mara kwa mara kwani utakuwa angalau unazijua timu unazobashiri uwezo wake. Unaweza kufuatilia kujua pia ligi cha nchi mbalimbali kujua huwa zinapenda kutoa matokeo ya namna gani, hii itakusaidia namna ya kuchagua betting zako kwani kuna option nyingi. Kwa mfano unawezajua timu za mpira wa miguu A na B huwa zikutana lazima kadi nyekundu iwepo kwa hiyo unaweza bet mechi ya leo kadi nyekundu itakuwepo. Au timu D na C huwa zinafungana magoli mengi kwahiyo ukaamua kubet labda mechi ya leo itakuwa na jumla ya magoli 3 au 4 nakuendelea.

SOMA NA HII:  Jinsi ya kurudisha Mafaili Yaliyofutwa Katika Kompyuta
  • Cheza mechi chache kwa siku unazoamini

Cheza kwa kiasi mchezo huu. Usiwe na tamaa kwamba unaweza pata pesa nyingi kwa mara moja kwahiyo ukacheza hovyo bila mpangilio, utaumia.

Hii ni kwasababu unapoweka mechi nyingi katika mkeka mmoja unapunguza uwezekano wa wewe kushinda. Japo kuwa wengi wanawaza kupata hela nyingi lakini wanasahau kuangalia uwezekano wa kushinda. Ni kweli kwamba ukiweka mechi nyingi ndio hela inaongezeka ila uwezekano wakushinda unapungua.

  • Usibashiri kwa mapenzi ama ushabiki

Usibet timu kwa sababu ya ushabiki: hiki ni kitu cha kuzingatia kwani wengi wwamekua wakibet kwa sababu tu ya mapenzi ya katika timu fulani.  Angalia uwezo wa timu yako dhidi ya timu pinzani kama inaweza shinda na hii itakuwa rahisi endapo utakuwa mfuatiliaji mzuri pia wa ligi ama mchezo unaobashiri.

Usiuchukulie serious sana huu mchezo na wala usiruhusu ukutawale sana ufanye kama ziada hakika utaufurahia.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA