Jifunze Njia Mbalimbali Za Kushusha Video Kutoka Youtube bure


Wengi wetu tunapenda kuangalia video za youtube kwenye simu na kompyuta, na tunatamani kuwa na baadhi ya video tunazozipenda ili tuweze kuzitazama tena na tena hata pale ambapo hatuna mawasiliano ya intaneti.  Ondoa shaka kwa maelezo yafuatayo utajua ni kwa namna gani unaweza kuzishusha video za youtube kwa vifaa/simu za android na kompyuta.

Jifunze Njia Mbalimbali Za Kushusha Video Kutoka Youtube bure

Zifuatazo ni njia mbalimbali za kukuwezesha kushusha (Download) video mbalimbali kutoka Youtube na hata mitandao mingine. Nitajaribu kuelezea njia mbalimbali hasa extensions, kutumia programu (softwares) au tovuti ambazo utaweka link kisha zenyewe zitakusaidia.

Kwa Kutumia Mtandao.

ClipConverter

ClipCoverter ni mtandao unaokunaweza kushusha video mbalimbali kutoka mitandao mbalimbali. Unachotakiwa kufanya ni kwenda na kukopi anuani (pale kwenye www.yo……) ya video unayoitaka.Ukishaikopi unarudi kwenye mtandao huu wa ClipConverter na kuiweka kwenye ‘Media Url Download’ na kushusha na kumbuka unaweza ukachagua aina ya mfumo (format) unaitaji. Hii inaweza kuwa MP3, MP4 3GP na zingine.

Muonekano wa sehemu ya kushusha-ClipConverter

 KeepVid

KeepVid nayo ni kama ClipConverter unaweza shusha video kupitia kuweka anuani ya video hiyo kwenye mtandao huo. Utofauti wake na ClipConverter ni kuwa KeepVid haina chaguo la mifumo mbalimbali.

Extension
Ni njia rahisi, hii ni kwa wanaotumia wa browser ya mozilla nadhani ndio yenye extension nyingi zaidi. Unachofanya ni kuiwekea extension browser yako unayotumia. Mfano ukifungua browser yako ya mozilla unaenda sehemu ya menu kisha palipoandikwa Adds On na kutafuta kati extension zifuatazo ambazi kwa maono yangu ndio bora.

  • Download youtube video as MP4: Nzuri sana na haijawahi kunisumbua tatizo lake inashusha video yako kwa mfumo mmoja tu wa MP4, hivyo kama una matarajio zaidi ya MP4 inaweza isiwe nzuri kwako.
  • Youtube MP3: Inakuja kusahihisha udhaifu wa extension ya pili hapo juu kwa kupata MP3 lakini haina option nyingine zaidi ya MP3.
  • Download helper: Hii ni nzuri zaidi, inakwenda mbali zaidi ya yotube, unaweza kupata video kutoka kwenye sites nyingi sana. Unaweza kuweka kuweka kwenye browsers za Mozilla na Chrome

NB: Unaweza kuziweka zote nne kwa pamoja na kuchagua ipi utumie kulingana na muktadha wa wakati huo.

Kwa Kutumia Programu za Kompyuta

Kuna programu nyingi sana za kutumia ila nitakupa moja ambayo ni maarufu inapokuja kwenye sifa ya utendaji kazi na ni ya bure.

Freemake [Windows]
Freemake ni programu inayokupa uchaguzi mzuri wa kile unachotaka kushusha. Unaweza badili mfumo na hata kiwango cha ubora wa video ili kupunguza ukubwa wa faili.  Kuishusha kwenye kompyuta yako bofya hapa.

Muonekano wa Freemake

IDM
Baba lao, popote unapocheza video yenyewe inajitokeza (pop) na kama utapenda kuwa nayo video unayoangalia basi utapobofya na kuipata papo hapo. Ina uwezo wake mzuri wa ku-pause na resume download yako pale internet inaposumbua, kuzima PC na kadhalika. Udhaifu wake inauzwa hivyo itabidi ununue ama uipate kupitia njia za panya (Torrents).

Kwa Kutumia simu ya mkononi

TubeBox(iOS)

Hii ni kwa wanaotumia iPhones au iPads (ios). Kupitia TubeBox utaweza kutafuta na kuangaliza video mbalimbali kutoka Youtube na pia utakuwa na uwezo wa kuzishusha na kuweza kuzitazama tena hata bila huduma ya intaneti. Kushusha bofya hapa.

TubeMate(Android)

Hii ni app nzuri inayokuwezesha kutafuta na kushusha video mbalimbali kutoka Youtube. Na inafanya kazi kwenye simu nyingi za Android, kuishusha bofya hapa.

WonTube (Android)

WonTube ni njia nyingine kwa watumiaji wa simu au tableti za Android. WonTube inakuwezesha kutembelea mtandao wa YouTube ndani yake na utakapoitaka video yeyote kunasehemu ya kubofya ‘Download’ na video hiyo itashushwa na kuhifadhiwa kwenye simu yako. Kuishusha kwenye simu yako bofya hapa.

2 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA