Njia 7 rahisi kuboresha usalama wa kompyuta yako


Ni dhahiri kwamba usalama ni muhimu sana tunapotumia kompyuta zetu au smartphone. Kwenye mtandao, utapata mafunzo mengi kuhusu hili, maandiko marefu na ya kina kuhusu itifaki zote za usalama ambazo unapaswa kuzifuata ili kujikinga. Tumezungumza mara nyingi juu ya hili, kwa hiyo leo tutaingia katika maelezo: hapa chini utapata vidokezo 7 rahisi ambavyo vitakusaidia kuongeza usalama wako wa kompyuta.

1. Daima Vinjari (browse) kwa kutumia “Incognito mode” unapokuwa nje ya kwako.

Kuna siku nilikua safarini, nilitaka kutumia kompyuta hivyo ikanibidi nitumie PC ya umma kwenye hoteli na nilikuta na ukurasa wa Facebook wa mgeni aliyepita. Sio shida na sipendi kumsumbua mtu yeyote, kwa hiyo niliifunga bila kutazama, lakini fikiria mtu huyo aliyekuja kutumia baada ya mtalii angekuwa mtu ambaye alitaka kuchunguza kwa ukaribu  ukurasa huo !!!.

Wakati wowote unapokuwa nje ya nyumba yako, tumia hali ya incognito (Incognito mode) ya kivinjari chako ili kujiokoa mwenyewe kwenye matatizo. Hii inajumuisha PC kwenye chuo au vyuo vikuu, maktaba, hoteli au eneo lolote la umma na hata kompyuta za marafiki zako. Hata kama ni waaminifu, unaweza kuepuka mtu kutumia akaunti yako ya barua pepe kwa makosa ikiwa unasahau kubonyeza “logout,” kwa mfano.

2- Usizidishe matumizi ya antivirus

Pointi hii inaonekana inapingana, lakini utaona kwa nini sio. Suala ni kwamba tunaponunua kompyuta mpya, tunatamani kuilinda zaidi na antivirus, kupambana na spyware, nk, nk, usiende mbali sana na hii! Kumbuka kwamba PC zenye Windows 10 zinakuja na programu yao ya antivirus, na kama hujaipenda hiyo, unaweza kutumia nyingine, lakini moja tu!

Programu nyingi za antivirus za sasa (Avast, AVG, 360 Security…) zinajumuisha ulinzi wa kila aina ya vitisho, hata katika matoleo ya msingi au ya bure. Chagua moja na uiruhusu kufanya kazi yake, ikiwa inakutana na kitu cha ajabu, itakujulisha. Ikiwa una tatizo maalum, kuna programu nyingi kwenye mtandao zinaweza kutatua tatizo lako. Ikiwa jambo hili limetokea, unaweza kuchukua hatua kwa kuweka (installing) ufumbuzi maalum.

3- Usiache kufanya sasisho (updates)

Programu nyingi mara nyingi zinaomba kuongezwa (updated). Hii inamaanisha zitachukua muda mrefu kufunguka lakini … haina thamani kusubiri? Programu zilizofanyiwa “update” ni njia moja wapo ya kupambana na uvamizi, hivyo weka programu unazozipenda “up-to-date” na kama wamekuomba kuupdate, usiache kufanya hivyo! Mbali na hilo, isipokuwa tukiongea juu ya michezo (games), programu za kompyuta huchukua dakika chache tu kufanya “update”.

Katika kesi ya Windows, ni jambo lilelile. Updates sio kwajili ya kukuzuia, ili ni kwajili ya kuboresha utendaji. Tatizo ni kwamba, tofauti na programu, wakati Windows inasasisha (updates) inachukua muda. Ili kuepuka kupoteza muda, weka sasisha (updates) za Windows zifanyike wakati hutumii PC.

4- Badilisha password yako mara kwa mara

Ndiyo, najua ni jambo la kushangaza kubadili maelezo, lakini sio jambo zuri kutumia neno la siri la Gmail ambalo ulikuwa nalo wakati unafungua akaunti yako mwaka 2004. Ninapendekeza kubadilisha nywila kwa huduma kuu unazotumia kila miezi 6 au kila mwaka. Katika baadhi ya matukio, jukwaa lenyewe linaweza kukuomba kufanya hivyo, lakini majukwaa mengine hayana mfumo huo.

Katika hali hii, tumia huduma yako ya kukumbusha kumbukumbu na kalenda (Google Calendar, programu za kuandika mipango yako …) ili ziweze kukujulisha kufanya mabadiliko haya mara kwa mara kama unavyotaka.

Pia, tumia meneja ya nywila (passwords manager) ili usisahau chochote. Google Chrome ina meneja yake ya neno la siri, lakini ikiwa unataka usalama wa ziada, tumia programu nyingine.

5- Kumbuka kufanya “backing up” (karibu) kila siku

Nina hakika unafanya kazi na nyaraka kadhaa kila siku ambazo yatakuwa majanga ikiwa zimepotea. Hata kama unatumia programu zisizo za mtandao kama “Word” na una external hard-drive, sio rahisi sana kuunda backup ya mtandaoni ya kila faili muhimu unayohitaji. Ingawa kuna huduma nyingi, ningependa kuziongelea mbili ambazo ni bora: OneDrive na Dropbox. Zote, baada ya kuziweka kwenye PC yako, fungua faili ya kawaida kwenye mfumo wako ambayo inapakia (uploads) faili kwenye cloud. Kwa hiyo, chochote unachotaka kuhifadhi, unapaswa kuweka kwenye faili hiyo, ambalo linapatikana kutoka kwenye kifaa chochote kilichounganishwa (kama vile simu yako). Weka nakala ya mafaili muhimu wakati wote unapoyaboresha na utaweza kuepuka shida katika siku zijazo.

Ingawa naipenda Google Drive, ushirikiano wake na PC sio mkubwa sana. Ndiyo sababu ninapendekeza tu Google kwajili ya Picha. Ikiwa mara nyingi unapiga picha kwenye smartphone yako na hutaki kuzipoteza, hii ndiyo huduma bora kwako. Google Photos ina chaguzi nyingi zinazofaa kuzijua, bofya hapa ili uzione zote na ujifunze kutumia huduma hii kwa hatua fupi.

6- Usifanye malipo kwa kila aina ya njia

Mara ngapi kwa mwezi unafanya manunuzi mtandaoni? Mimi mara chache, mara nyingi sana, kusema ukweli. Ndiyo sababu lazima uwe makini kuhusu jinsi unavyolipa. Usitumie mbinu usizozifahamu za kulipa na daima chagua PayPal, Google Wallet au, ikiwa unalipa kwa credit card, hakikisha kuwa njia hii ya malipo ina “payment gateway,” yaani, mpatanishi kati ya kadi yako na muuzaji, ambayo inathibitisha taarifa zako hazitafikiwa moja kwa moja. Usiwe na hofu, hili linaonyeshwa wazi kwenye maduka ya mtandaoni.

Epuka kulipa kwa uhamisho wa benki kama inawezekana, kwani ikiwa kuna shida kwa ununuzi wako ni vigumu kudai na inategemea benki yako, bila shaka watakataa.

Je, unanunua na kuuza kwa watu binafsi na mtu anasisitiza kulipa kwa uhamisho wa benki (banking transfer) ? Ikiwa ni kiasi kidogo cha fedha na mtu anaaminika (kwa mfano, kuna maoni kwenye tovuti ambayo unanunua), ninaweza kusema ni sawa, lakini kwa upande mwingine, unaweza kuwahimiza wengine kujaribu PayPal, kwa kuwa ni bure kati ya watu binafsi na kufungua akaunti ni rahisi sana: unapaswa kuongeza akaunti yako ya benki (ambayo hutaiona kamwe).

7- Funga mlango wa uvumi kwenye Facebook, Whatsapp au barua pepe

Kwa hakika umeamini uvumi usio na msingi kwenye mitandao ya kijamii na kuushirikisha: kufanya hivyo huleta kelele na kuchanganyikiwa tu. Wakati mwingine unaweza hata kusababisha madhara makubwa, unaweza kuharibu maisha ya mtu! Ndiyo, wakati mwingine picha za wahalifu zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii ni za watu wa kawaida tu. Picha zao zina bahati mbaya ya kuangukia mikononi mwa watu wasio salama. Je! Ungependa hilo lifanyike kwako?

Kabla ya kushirikisha jambo lolote, chapisho au picha kwenye Facebook au Whatsapp, hasa ikiwa ni alarmist, kwanza fuatilia ukweli wa jambo kwa kutumia Google na, zaidi ya yote, utumie akili. Kwa mfano, kabla ya kushirikisha picha ya mtu aliyepotea, bofya kiungo cha awali (original link), kwa kuwa, kwa shukrani, mara nyingi mtu amewahi kupatikana. Na kama taarifa ni kutoka kwenye shirika linalojulikana, hesabu hadi 10 na fikiria … shirika linaweza kutumia WhatsApp kweli kueneza taarifa badala ya njia zao rasmi?

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA