KompyutaProgramu

Njia 5 za Kuchukua Screenshots kwenye Windows 10

Screenshots ni njia nzuri sana ya kuandaa na kushirikisha vitu vilivyopo kwenye skrini yako. Inaweza kuwa tweet ambayo unadhani mtu anaweza kuifuta. Uwezo wa kuhifadhi screen yako kwa matumizi mengine ni jambo muhimu.

Kwa bahati nzuri, kuna zaidi ya njia chache za ku-capture skrini unayotaka kuhifadhi. Kuna kitufe cha Print Screen, njia ambayo inatengeneza faili jipya kwajili yako, Programu ya Windows vya “Snipper Tool” na kama wewe unapenda kuchukua screenshots mara kwa mara, kuna programu za bure tunazoweza kupendekeza kwako.

1. Jinsi ya Kuchukua Screenshot ya Screen yako Yote

1. Gonga kifungo cha Print Screen kwenye kibodi yako. Picha ya skrini sasa itakuwa imehifadhiwa kwenye clipboard yako na unahitaji kuiweka kwenye graphics editor kama vile Windows Paint.

2. Andika “paint” kwenye search bar karibu na Start menu.

3. Chagua “Paint”

4. Bonyeza “Paste”

Screenshot yako iko tayari!

2. Jinsi ya Kuchukua Screenshot ya Active Window

1. Bonyeza Alt + Print Screen.

2. Andika “paint” kwenye search bar karibu na Start menu (kama Paint imefunguliwa yatari, click Control+N kisha bonyeza OK wakati Paint inakuomba uidhinishe urefu na upana).

3. Chagua “Paint”

4. Bonyeza “Paste”

Screenshot yako ipo kwenye window unatakiwa kuifungua ili ifanye kazi!

3. Jinsi ya Kutengeneza Screenshot File bila ya kutumia Programu yoyote

1. Bonyeza Windows key + Print Screen.

SOMA NA HII:  Makosa 10 ya kawaida ambayo yanaweza kuharibu Laptop yako [Muhimu Kusoma]

Unapotembea kwenye folda ya Screenshots ndani ya Picha zako, screensh0t yako itakuwa huko!

snipping win02 w10

4. Jinsi ya Kuchukua Screenshot ya Sehemu maalum ya Screen yako

1. Andika “snipping tool” kwenye search bar karibu na Start menu.

2. Chagua “Snipping Tool”

3. Bonyeza “New”

4. Bonyeza na kisha drag mshale (cursor) kuchagua eneo la skrini unalotaka kutumia; achia mshale(cursor) mara baada ya kuchagua eneo unalotaka kucapture.

Screenshot itafunguliwa katika Snipping Tool!

5. Jinsi ya Kuchukua Screenshots Kwa maujanja Zaidi

1. Fungua PicPick download page, na kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa “Free Download”

2. Fuata melekezo ku-install PicPick, na utapata orodha ya njia maalum za ku-capture sehemu au skrini yako yote. Bonyeza “Scrolling Window” itakuwezesha kucapture kurasa nyingi kadri unavyoweza kupitia, badala ya toleo tuli la window.

3. Kuweka (instal) PicPick itabadilisha amri muhimu ya kompyuta yako kwajili ya viwambo vya skrini(computer key commands for screenshots), kwa hivyo unapaswa kuzijua amri hizo. Bofya kwenye “Show hidden icons” kwenye kona ya chini ya kulia ya skrini yako.

screenshots 3rdparty03b w10

4. Bonyeza kwenye icon ya PicPick.

screenshots 3rdparty04b w10

5. Chagua “Program Options”

screenshots 3rdparty05b w10

6. Chagua “Hot keys” kutoka kwenye Orodha ya mkono wa kushoto

screenshots 3rdparty06b w10

Hapa unaweza kuona default key commands zilivyo sasa ulivyoweka PicPick, na pia kuzibadilisha kulingana na mahitaji yako.
screenshots 3rdparty07b w10

SOMA NA HII:  Mifumo maarufu zaidi ya uendeshaji "operating systems" kwenye simu na kompyuta
Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.