Nyingine

‘Nimemruhusu Ronaldo Kucheza Nafasi Anayopenda’- Kocha wa Madrid Zidane

Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane, amethibitisha kwamba amemruhusu Cristiano Ronaldo kuwa huru, na kuchagua nafasi yoyote anayopenda kucheza wakati wa mechi.

Ronaldo alifunga goli lake la 99 na 100 katika mashindano ya Ulaya, kwa kufunga mabao mawili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Bayern Munich katika Ligi ya Mabingwa siku ya Jumatano.

Goli la kwanza alifunga kwa kumalizia “cross” iliyotoka kwa Dani Carvajal , kabla ya kupiga mkwaju karibu na goli na mpira kupitia miguu mwa Manuel Neuer.

Nahodha wa Ureno alianza mechi akitokea kushoto, huku Karim Benzema akicheza kati. Lakini alimaliza kama mshambuliaji wa kati baada ya mshambuliaji wa Ufaransa kutoka.

Baada ya mechi zidane alisema:

“Cristiano knows where his position is,”

“He knows when to play centre-foward or on the left. The positions he takes, and where he scores his goals – that’s all him.”

SOMA NA HII:  Unatumia "Lock ? " ya aina gani kwenye simu yako?

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako