Sambaza:

Kiungo wa klabu ya Chelsea Ngolo Kante ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa chama cha wachezaji wa kulipwa nchini England PFA kwa msimu wa 2016-17.

Kante amewapiku nyota wengine wa ligi hiyo Eden Hazard, Harry Kane, Romelu Lukaku, Zlatan Ibrahimovic na Alexis Sanchez waliokua wakiwani tuzo hiyo pia.

Takwimu za N’golo Kante msimu huu akiwa na Chelsea katika EPL

Kiungo wa Tottenham Dele Alli, ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi kwa mwaka wa pili mfululizo. na kuwapiku Michael Keane wa Burnley, Romelu Lukaku, kipa wa Sunderland Jordan Pickford na Leroy Sane wa Manchester City walikua wakiwani tuzo hiyo ya mchezaji chipukizi wa mwaka.

Lucy Bronze wa Manchester City ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa kike wa mwaka katika hizo, huku Jess Carter anayechezea Birmingham ameibuka kidedea kwa kuwa chipukizi bora kwa upande wa wanawake.


Sambaza:
SOMA NA HII:  Nahitaji Antivirus, Je Wewe Unatumia Antivirus Gani Kwenye Kompyuta Yako?

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako