Home Nyingine News Alert: Tundu Lissu akamatwa akiwa Mahakamani Kisutu

News Alert: Tundu Lissu akamatwa akiwa Mahakamani Kisutu

0
0

Mwanasheria Mkuu wa Chama Tundu Lissu amekamatwa na Jeshi la Polisi muda mfupi uliopita na anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kati Jijini Dar es Salaam. Hadi sasa polisi hawajasema sababu ya kumkamata na kumshikilia Tundu punde tu baada ya kutoka Mahakama ya Kisutu ambako kesi dhidi yake kuhusu tuhuma za uchochezi ilikuwa imefutwa na mahakama hiyo.

Lissu alikuwa amefika mahakamani hapo katika kesi ya kuchochea vurugu ambapo alituhumiwa kuwa Januari 11, mwaka huu katika kampeni za uchaguzi jimbo la Dimani aliwashawishi watu wasiridhike na wawe na nia ovu dhidi ya utawala.

Aidha, Lissu aliachiwa baada ya upande wa Jamhuri kuwasilisha hati ya kuondoa shtaka hilo mahakamani chini ya kifungua namba91 (1) cha makosa ya jinai akionyesha DPP hana haja ya kuendelea na kesi, mahakama ikaridhia na kumuachia.

(0)

LEAVE YOUR COMMENT

Your email address will not be published. Required fields are marked *