Netflix sasa ina wanachama milioni 125


Netflix imetoa matokeo yake ya kifedha kwa robo ya mwaka 2018, ambayo yanaonyesha kampuni hiyo imepata faida ya dola 3.6 bilioni katika mapato ya Streaming kutoka kwa wanachama wake milioni 125.

“Kazi yetu ni kutumia fedha hii kwa busara ili kuongeza furaha kwa wanachama wetu,” – Netflix.

Mapato ya Netflix yanakuwa kwa 43% mwaka baada ya mwaka katia Q1, hii ni kasi kubwa zaidi katika historia ya biashara yake ya streaming.

Ukuaji huu umetokana na ongezeko asilimia 25 katika kulipia uanachama wa wastani na kuongezeka kwa asilimia 14 kwa wastani wa bei ya kuuza.

Katika robo ya mwaka, Netflix imeongeza washiriki (subscribers) milioni 7.41.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *