Tech Poll

Unaikadiliaje Mozilla, Samahani, Nembo Mpya ya Moz://a: 😊 au 😕 ?

Mozilla, shirika lisilo la kiserikali linalosimamia na kuendesha Firefox limefanya mabadiliko makubwa ambayo yamebadiliko karibu kila kitu, namaanisha, nembo, font, color palette, usanifu wa lugha, na picha.

Tukiangalia mabadiliko yaliyofanyika: Nembo ya kampuni hii ndiyo inazungumziwa zaidi. Sasa herufi “ill” kwenye jina la Mozilla zimebadilishwa kwa kuweka koloni na mikwaju inayounda anwani ya tovuti yoyote ile. Kwa maneno mengine Mozilla sasa ni Moz://a. Rangi pia imepokea mabadiliko pamoja na kuwa na mpango mpya ambao umezingatia “highlight colors” zinazotumika kwenye Firefox pamoja na browsers nyingine. (Unaweza kusoma zaidi kuhusu mabadiliko mengine hapa.)

Turudi kwenye Nembo(logo), hii ni nembo ya zamani:

… Na mpya ni hii:

Siwezi kuamua kama nembo mpya ina mwonekano mzur: ama ni mbaya. Kwa hiyo, nimeleta mada hii kwenu wadau.

😊 au 😕?

Zinazohusiana

Toa Maoni Hapa:

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako