Intaneti

Nefrids Africa Imeshinda Seedstars Dar Es Salaam Edition 2017

Tanzania Nefrids Africa, inayoendesha SimuBima, Suluhisho la Bima kwa njia ya Simu za mkononi iliyoundwa kuwafikia watumiaji wengi zaidi nchini Tanzania kwa kutumia njia za digital mwezi wa Julai 20 ilishinda Seedstars Dar Es Salaam na itawakilisha Tanzania kwenye Seedstars Summit nchini Uswisi kushindania zaidi ya dola milioni 1 katika uwekezaji wa usawa na zawadi nyingine.

Nefrids Africa itashiriki katika Seedstars Summit, itakayofanyika Uswisi mwaka 2018, inafanyika kwa kipindi cha wiki moja kukiwa na fursa ya kukutana na washindi wengine 75 kutoka duniani kote, pamoja na wawekezaji wa kimataifa na washauri.

Siku ya mwisho ya Mkutano itafanyika mbele ya watazamaji zaidi ya 1’000 waliohudhuria kushindania hadi dola milioni 1 katika uwekezaji wa usawa na zawadi nyingine.

SomaApps na suluhisho lake la simu za mkononi kuorodhesha na kuchanganya wanafunzi na maelfu ya Udhamini wa ndani na wa kimataifa (domestic and international scholarships) ilikuwa ya pili, na Worknasi na jukwaa lake la mtandao wa ofisi ilishika nafasi ya mwisho katika 3 juu.

Startups nyingine zilizokuwa zimealikwa ni Kampuni ya TanzDevs, ScholarDream, HadithiApp, Flow Farm, Emakatt, Be A Lady, na Afropremiere.

Seedstars iliandaa tukio hilo kwa msaada wa Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania, COSTECH, Human Development Innovation Fund (HDIF), Buni Hub, pamoja na Enel Green Power.

Seedstars World itakayofata itafanyika Kampala kuchagua kampuni za kiteknolojia inazorahisisha huduma mbalimbali nchini Uganda. Seedstars World inatafuta startups zenye ubunifu ambazo zinatatua masuala ya kikanda na / au kuendeleza bidhaa zenye faida kwa soko la kimataifa.

SOMA NA HII:  (Kama Ilivyotarajia) Kwa Mwaka 2017, Zaidi ya Nusu ya Emails Dunia Nzima Zimefunguliwa kwanza kwenye Simu ya Mkononi.

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.