Home Nyingine Nash Mc: Kabla hujalilia mabadiliko fikiria kuhusu familia yako,dada zako na vizazi vijavyo

Nash Mc: Kabla hujalilia mabadiliko fikiria kuhusu familia yako,dada zako na vizazi vijavyo

0
0

Jumapili tarehe 19/3/2017 rasmi Nash Mc ataachia wimbo wake mpya unaitwa SHUJAA amemshirikisha Mau Kolimba, mdundo umetengenezwa na Sallii Teknik .

Muimbaji huyo wa Hasi 15 kupitia mitandao ya kijamii amezungumza kuhusu mabadiliko ndani ya utamaduni wa HipHop na watu wanaotaka mabadiliko.

“Watu mnaolilia mabadiliko katika utamaduni wa Hip Hop mpo sahihi kwa mitazamo yenu,lakini niwakumbushe tu kua kwa kufanya hivyo mnaungana na ulimwengu wa Mabepari na Utandawazi katika kukandamiza haki za watu wa tabaka la chini, mnapaswa kujiuliza kwa nini mabepari wanataka tuzungumze lugha 1 ya ushetani,kama Ushoga,usagaji na wanawake kuvaa wanavyotaka vitu ambayo vipo kinyume hata na maandiko ya dini zetu.”

“Tafakari kwa makini kwa nini Tamaduni zote au kundi la watu au mtu ambae anapigania ukweli na kuongea mambo chanya kwa ajili ya jamii anapigwa vita na mabepari? Mabepari hawataki tuamke,mabepari walimuua hayati 2Pac Shakur kwa kupigania ukweli na tukaaminishwa magenge ya Big yalimuua Pac na baadae magenge ya Pac yalimuua Big, na hakuna aliekamatwa katika kesi ya mauaji hayo.”

“Naamini Utamaduni wa Hip Hop katika kuleta mabadiliko chanya na kupingana na tamaduni zingine zote zinazopotosha ulimwengu. Tusililie mabadiliko ambayo hatujui madhara yake,sio kila utamaduni utakwenda na wakati, mnaotaka kwenda na wakati mpo tayari kuona Kuna haki za Mashoga,Wasagaji na haki zingine za kishetani? Kabla hujalilia mabadiliko ndani ya Utamaduni wa Hip Hop fikiria kuhusu familia yako,dada zako na vizazi vijavyo ambavyo Hip Hop inaendelea kuwapigania tangu na yangu.”

“Ukubwa unaambatana na kutetea yaliyo chanya katika jamii yako na sio kushiriki kwenye upotoshaji na haijalishi umefanya hivyo mara ngapi. Elimu ni pana na watu wanahitaji kujifunza kila siku.”

LEAVE YOUR COMMENT

Your email address will not be published. Required fields are marked *