Nyingine

Nash Mc-HAKUNA MAPENZI WALA KARIAKOO MUBASHARA

Nash Mc ni msanii wa hiphop ambaye amekuwa mstari wa mbele kwenye mapambano ya kukuza na kueneza Kiswahili  ni moja kati ya wasanii wachache wanaotumia kiswahili fasaha kwenye nyimbo zao.

Baada ya hivi karibuni kuibuka matumizi ya neno Mubashara, Nash Mc kupitia tamasha lake la KINASA (Kiswahili na Sanaa) aliamua kutoa maana na matumizi sahihi ya neno hilo:

Kupitia Mtandao wa instagram Nash Mc ameandika:

KUMEKUCHA NA MAKUCHA YAKE.
Muda si mrefu nimefika kituo cha basi cha Buza Kanisani nasubiri gari za kuelekea Kariakoo, mara namsikia Konda anasema, KARIAKOO MUBASHARA,KARIAKOO MUBASHARA hiyooooo, Zaidi ya mara 3, nikajiuliza huku BUZA nilipohamia kila siku napita lakini sijawahi kusikia kuna kituo kinaitwa MUBASHARA au KARIAKOO imeongezewa jina mbele?? Nikajiuliza.

Baada ya kupanda nikamuuliza Konda,KARIAKOO MUBASHARA maana yake nini?? Akaniambia Kariakoo Moja kwa Moja hii baba bila ya chenga. Nikatabasamu huku moyoni nikiumia kuona msamiati huu MUBASHARA ukianza kutumika katika muktadha au maeneo yasiyostahili, Radio,Runinga na magazeti yamepotosha kwa nguvu na sasa jamii inaanza kupokea upotoshaji huo kama ndio usahihi.

Kwa kweli tunarudisha nyuma nguvu za wapigania maendeleo ya lugha yetu ya Kiswahili kwa maksudi kabisa. Nchi jirani zinaanza kuweka mikakati ya kuendeleza Kiswahili lakini sisi wenye lugha yetu tunakesha kupotosha jamii kuhusu matumizi sahihi ya maneno ya KISWAHILI.

Napinga na nitaendelea kupinga kwa nguvu zangu zote nikiwa hai upotoshaji huu wa lugha yangu na hata upotoshaji mwingine wowote unaohusu utamaduni wangu.

Nimezoea kuambiwa najifanya najua,nna wivu,chuki na majungu,lakini kwangu daima ntasimama katika yale nayoyaamini sitosikiliza maneno ya wapumbavu wanaoamua kupotosha jamii kwa nguvu na ushawishi waliokua nao.

HAKUNA MAPENZI WALA KARIAKOO MUBASHARA.

NDIMI MSWAHILI MSHAIRI NASHIR.
SAUTI YA WANYONGE.
TITI LA MAMA LITAMU HATA KAMA LA MBWA.
KISWAHILI LUGHA YANGU.

Tazama Video hapa chini:

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *