Namna ya Kuchapisha Blog yako Mtandaoni


Tumekwisha anzisha blog kwa mafanikio hadi sasa kama ulifuatilia mafundisho yetu tangu mwanzo. Hatua ya mwisho kwenye blog ni kuifanya iwafikie watu wote ulimwenguni, ili uweze kupata wasomaji zaidi na kupata umaarufu. Sasa tunaelewa kuwa wanablogu wengine huanzisha blogu zao kwa matumizi ya kibinafsi, kwa hivyo tutazungumzia jinsi ya kufanya makala zako kuwa za kibinafsi (private blog articles ) zisisomwe na watumiaji wasiohitajika.

Kitu cha kwanza unachotakiwa kufanya mara moja baada ya kuchapisha blogu yako ni kuhakikisha kuwa inaonekana kwa watumiaji wote wapya kupitia injini za utafutaji kama google, na nyinginezo. Kwa hiyo utatakiwa kwenda kwenye sehemu ya WordPress admin panel inayoitwa Settings > Reading kisha nenda sehemu iliyoandikwa Search Engine Visibility

Utaona ukurasa unaoonekana kama screenshot hiyo hapo juu. Ikiwa unatafuta kuchapisha blogu yako kwajili ya ulimwenguni usiweke alama ya tiki kwenye kisanduku cha Discourage search engines from indexing this site. Kwa kufanya hivyo, utaona blogu yako inaonekana katika injini za utafutaji kama google, yahoo, technorati, na nyinginezo. Ikiwa unataka blogu yako ionekane kwako tu (ni jambo linaloeleweka kabisa kwa blogu za kibinafsi na diary), weka alama ya tiki kwenye sehemu hii”.

Hiyo ni hatua ya kwanza ya kuchapisha blogu yako kwa ulimwengu. Sasa hatua ya pili kufanya ifanye kazi kwenye mitandao ya kijamii kama vile Twitter, facebook, stumbleupon, reddit, digg, na mingine mingi. Jiunge nao na uitumie kwa faida yako.

Mfano wa kutumia Twitter ni kushirikisha makala zako kwenye Twitter na marafiki zako. Ni wazi, utapata marafiki  ikiwa unachangia mada mbalimbali za jumuiya na unashiriki kutoa maelezo muhimu. Unaweza pia kushirikisha stori zako kwenye digg, na mitandao mingine ya kijamii.

Kumbuka tangaza stori ambazo ni muhimu tu. Usiombe marafiki zako kusanbaza kila kitu chako kwa sababu si kila makala yako ni nzuri.

Unaweza pia kushirikisha links na wanablogu wengine ambao wako katika niche sawa na wewe. Unaweza kuwapata kwenye google, technorati, au majukwaa ya mtandaoni, kama wewe ni mwanachama. Jaribu kushikamana, na unaweza kupata backlinks kutoka kwenye tovuti nyingine ambazo ni muhimu sana kwa ukuaji wa blogu yako.

Sasa kwa wale watumiaji ambao hawataki machapisho yao kuonekana kwa watu wengine, kuna njia zaidi za kulinda posts zako za blog ambayo tutakushirikisha hapa.

Njia moja wapo ni kutumia nenosiri kulinda machapisho yako. Ni hatua rahisi sana. Unapoandika chapisho jipya, kabla ya kuchapisha angalia sehemu ya kulia ya ukurasa. Ambapo inasema publsih. Huko utaona chaguo ambalo linasomeka, Visibility: Public (Edit), bofya sehemu hiyo na utaona chaguo kama ilivyo katika picha hapa chini:

Chagua chaguo la nenosiri, na utengeneze nenosiri lako, kwa njia hii unaweza kuwa na nenosiri la machapisho yako binafsi. Na watumiaji wanaweza kuona, ikiwa wana nenosiri. Kumbuka kwa kuzuia injini za utafutaji  kuona chapisho lako watu bado wanaweza kuja kwenye tovuti yako na kusoma machapisho yako, kwa hiyo hii ni mojawapo ya njia ambazo unaweza kuwa na usalama wa 100%.

Sasa ikiwa unataka tu kushirikisha blogu yako kwa watu fulani, njia bora ni kuwa na ulinzi wa nenosiri (password protection). Kwa mfano, wakati mtu anapoandika domain yako xxx.com, wataona sehemu ya kuingia (login). Ili kufanya hivyo unatakiwa kuwa na Cpanel Hosting, ili uweze kutumia kipengele cha ulinzi wa nenosiri.

Tafuta Cpanel Hosting, kutoka sehemu yoyote, na tutumie barua pepe, tunaweza kufanya mchakato kwa ajiri yako.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA