Namna ya Kubet na Maana ya “Betting Options” Katika Mpira


Watu wengi wakisikia neno bet, moja kwa moja wanahuisha na mpira wa miguu, ni kweli wapo sawa ila betting siyo kwenye mpira wa miguu tu hata kwenye michezo kama cricket, basketball, ngumi na michezo mingine. Leo tungalie kubet kwa upande wa mpira wa miguu ambao unaongoza kwakua na mashibiki wengi duniani.

Full Time Result

Hii ni matokeo ya mechi kwa dakika 90. Inaweza ikawa 1 (Timu ya nyumbani kushinda), X (Draw/Sare) au 2 (Timu ya ugenini kushinda). Kwa mfano: Chelsea vs Liverpool na chaguzi (option) zipo 1 X 2 hii ina maana kwamba ukichagua 1 ni kwamba timu iliyo nyumbani ambayo ni Chelsea ishinde, ukichagua X ina maana timu zitoke sare na ukichagua 2 ina maana timu iliyopo ugenini ambayo ni Liverpool ishinde.

Over/Under 2.5

Ukichagua Under 2.5 hii ina maana kwamba katika hiyo mechi magoli yatakayofungwa yasizidi mawili, yaani iwe ni kuanzia 0 na yasizidi mawili. Hii haijalishi nani kamfunga mwenzake ili mradi tu jumla ya magoli yasizidi mawili hata kama wakifungana 1-1, 0-1, 0-2 au 0-0 ni sawa. Na kama ukichagua Over 2.5 ina maana hiyo mechi izae magoli zaidi ya mawili, yaani kuanzia 3 na kuendelea na pia haijalishi nani kafunga au wamefunganaje.

SOMA NA HII:  Jinsi ya kudownload picha na video kwenye status ya mtu WhatsApp

GG and NG

GG ina maana kwamba timu zote katika mchezo zitapata goli. Haijalishi watafungana ngapi na kwa uwiano gani, ili mradi tu kwa kila timu itafunga goli hata ikiwa 1-1, 1-2, 5-3 ili mradi kila timu iweze kumfunga mwenzake. NG ina maana kwamba mojawapo ya timu haitafunga goli au timu zote hazitafunga goli.

DRAW NO BET [DNB]

Hii ina maana kwamba endapo timu zitatoka sare kutakuwa hakuna bet yaani utarudishiwa pesa yako uliyobet kwenye hiyo mechi. Kwa mfano inacheza Chelsea vs Liverpool na wewe ukachagua Chelsea DRAW NO BET hii ni kwamba Chelsea akishinda na wewe utakuwa umeshinda bet yako, Chelsea akitoka sare ni kwamba hakuna bet hapo hivyo utarudishiwa fedha yako uliyowekeza na endapo Chelsea atapoteza huo mchezo nawe utakuwa umepoteza pesa yako. Hivyo ndivyo itakavyokuwa pia endapo utachagua Liverpool.

Double Chance

Ikiwa 1X ni kwamba utashinda endapo timu iliyopo nyumbani itashinda au itatoka sare. Ikiwa 12 ni kwamba utashinda endapo timu mojawapo itashinda hajalishi nani kashinda ili mradi tu timu moja ishinde na sio sare. Ikiwa 2X ni kwamba utashinda endapo timu iliyo ugenini itashinda ama itatoka sare.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA