Nahitaji Antivirus, Je Wewe Unatumia Antivirus Gani Kwenye Kompyuta Yako?


Siku hizi kuna mamia ya antivirus na kila mtu anasema antivirus flani ni bora kutokana na uzoefu wake na jinsi anavyotumia kompyuta kuhakikisha usalama wake kulingana na mazingira aliyopo. Kwa njia moja ama nyingine hakuna antivirus ambayo ni bora zaidi.

antivirus

Ila kuna antivirus ambazo majina yake ni maarufu na watu wengi wanapenda kuzitumia. Miongoni mwa antivirus zinazotumiwa na watu wengi ni Avast, Nod, avira, AVG, Kaspersky, Microsoft security essentials na nk.

Bila shaka kila mtu ana chaguo lake.

SOMA NA HII:  Vita ya Facebook na Marekani, Mambo 6 Yanayotarajiwa

Sasa, kwa faida ya kila mtu tuambie wewe unatumia antivirus gani kwenye kompyuta yako, pia kumbuka kutoa sababu za kutumia antivirus hiyo na ufanyaji kazi wake upo vipi ili tuweze kujifunza ni antivurus gani inafanya kazi vizuri kwenye kompyuta za watu wengi.

Je antivirus unayotumia haifanyi kompyuta yako kuwa nzito na vipi kuhusu ubora wake ? tangu umeanza kuitumia ina uwezo gani wa kupambana na virusi ?

Tuambie unatumia Antivirus gani kwenye kompyuta yako ?

Je, Antivirus gani nzuri zaidi ?

Toa maoni yako hapa chini.

Unaweza kutueleza kama kuna antivirus ulikua unaitumia lakini sasa umeachana nayo na kuanza kutumia nyingine, kumbuka kuandika sababu za kwanini uliacha kutumia antivirus hiyo.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA