Sambaza:

Kadri siku zinavyozidi kwenda Teknolojia nayo inakua na kurahisisha mambo zaidi, sasa mtu wangu wa nguvu ikufikie hii toka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Serikali Mtandao Dkt. Jabiri Bakar.

Dr. Jabiri ametangaza mfumo mpya wa Tehama ambao utamfikishia mwanafunzi aliyemaliza chuo taarifa za ajira punde tu zinapotokea kwa kupitia simu yake mkononi.

Ameelza kuwa mfumo huu utapatikana kwenye simu za aina zote na mwanafunzi yeyote atakayekuwa ameweka taarifa zake zote kwenye mfumo huu atatumiwa ujumbe wa nafasi za kazi zilizotangazwa kwenye ofisi za Umma.

Pindi tu ajira zinapotangazwa, mfumo huu unapitia taarifa zote za wanafunzi na kwa wale ambao taarifa zao zinaendana na ajira zilizotangazwa wanatumiwa ujumbe mfupi katika eneo lolote walilopo nchini,” -Dr. Jabiri

SOMA NA HII:  Simu nzuri zinazouzwa kwa bei nafuu Tanzania

“Baada ya mchakato huu, ikifika siku ya mwisho wa tangazo hilo la kazi mfumo unatoa majina yote ya ambao wameomba nafasi hiyo ya kazi” -Dr. Jabiri

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako