myPlan app kuwaepusha wanawake katika manyanyaso ya wapenzi wao Afrika


App mpya ya simu janja iliyotengenezwa ili kuwasaidia wanawake kukabiliana na masuala ya unyanyasaji wa kijinsia inakaribia kuzinduliwa kwenye nchi za Afrika.

Muonekano wa App ya myPlan. Picha kwa hisani ya THOMSON REUTERS FOUNDATION

App hiyo imetengenezwa ili kusaidia wanawake kutambua kama wanateswa na wapenzi wao kwenye mahusiano ili wajiepushe na mahusiano hayo kwa usalama.

App hiyo inayojulikana kama Myplan imetengenezwa na watafiti wa Jimbo la Baltimore Marekani katika Shule ya Uuguzi katika Chuo Kikuu cha Johns Hopkins. App hiyo ina watumiaji 10,000 nchini Marekani na inapatikana pia Canada, Australia na New Zealand lakini bado haijafika barani Afrika.

Nancy Glass, profesa anayeongoza mradi wa MyPlan, alisema maoni mazuri tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2016, pamoja na pengo la habari juu ya manyanyaso ya wapenzi barani Afrika, imewashawishi kufanya upanuzi – kwanza Kenya, halafu Ghana na Somalia.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *