Mwongozo wa Kuboresha WordPress Kwa Watumiaji Wapya [Infograph]


Kuwa na toleo la sasa la WordPress ni muhimu kwa usalama wa blogu yako. WordPress blog imechukua hatua kali kwa kusisitiza kwamba watumiaji lazima waboreshe (upgrade) blogu zao kwa sababu za usalama. Kwenye makala hii tumekusogezea infograph inayohusisha utafiti uliofanywa na Syed zaidi ya miaka miwili kuhusu blogs za WordPress zilizokuwa hacked. Hii infograph pia inaonyesha mwongozo wa hatua kwa hatua ili kuboresha WordPress.

Watu wengi hujisikia vibaya  kuboresha (upgrade) kwa sababu Plugins zitaharibika na tovuti haiwezi kufanya kazi vizuri. Lakini ni bora kurekebisha tatizo dogo, au ni bora kufanya tovuti yako iwe rahisi kuvamia, kisha urejesha kila kitu, na kuboresha na kurekebisha kila kitu baadaye. Ni bora ikiwa unachukua njia ya kwanza kwa sababu itakuwa rahisi na utaokoa muda.

Hii inapaswa kuwa mwongozo wako wa kumbukumbu wakati wote unapotaka kuboresha blogu yako ya WordPress. Tunapaswa kusisitiza kuwa ni muhimu sana kutumia toleo la hivi karibuni.

Ingawa hii sio hatua pekee ya kuongeza usalama, hii hakika ni mojawapo ya hatua muhimu zaidi. Ikiwa unataka kujua jinsi gani unaweza kulinda blogu yako ya WordPress, angalia post yetu ya usalama wa WordPress.

Watu wengi hawana umakini kwenye plugin upgrades, lakini Plugins inaweza kuwa na athari kubwa katika usalama wa blogu yako. Kila mara msanidi programu (developer) anatoa sasisho, pia hutoa bug fix report. Mara nyingi, hutaja baadhi ya matatizo ya kiusalama ambayo yamerekebishwa. Sasa wakati hacker anaona kwamba unatumia toleo la zamani la Plugin, tayari wanajua jinsi ya kuvamia tovuti yako. Usifanye kazi yao iwe rahisi. Boresha sasa.

Ikiwa una mapendekezo yoyote kwa watumiaji wapya ambao wanaboresha blogu yao ya WordPress, tafadhali andika kwenye eneo la maoni.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA