Sambaza:

Hatujui kama kuna watu wengi ambao wataikumbuka Adobe Flash. Kwa sababu HTML ina kasi, salama zaidi, na rahisi kuiboresha. Flash haina umaarufu mkubwa siku hizi. Mwaka wa 2014, zaidi ya 80% ya watumiaji wa Chrome walitembelea tovuti na Flash, lakini hilo ni anguko la asilimia 17% na inaendelea kushuka.

kuongezeka kwa matumizi ya smartphone.

Habari za hivi karibuni ni kwamba Adobe itasitisha support kwa Plugin hii mwaka 2020, na Google ina mipango yake yenyewe kuhusu support ya Flash kwenye Chrome. Plugin itaondolewa kabisa mwaka 2020, lakini kuna mengi zaidi ya kufanya kwa sasa tunapoelekea kwenye mwisho wa maisha ya Flash. Katikati ya 2018, Chrome itaomba ruhusa kwa mtumiaji kabla ya kuendesha (run) Flash (huu ni mfumo mzuri kuwanao). Na katikati ya 2019, Plugin itazimwa lakini bado itabaki kwenye Chrome. Vivinjari vingine vina mipango sawa.

SOMA NA HII:  Google itahamasisha wafanyakazi 10,000 kuboresha video za YouTube

Huku Flash ikiwa inapotea taratibu kwenye intaneti na ni muda mrefu tangu ipotee kwenye simu, huu ndiyo mwisho wa mstari wa programu. Hatuwezi kusaidia lakini tunajisikia vibaya tufikiria juu ya michezo yote midogo (mini-games) tuliyocheza enzi za utoto wetu, lakini kukua kwa teknolojia kumesababisha yote haya. Hebu tuambia unafikiria nini ama una maoni gani kuhusu habari hii!

kuongezeka kwa matumizi ya smartphone.

Google wanasema kuwa matumizi ya Flash kwenye Chrome yameshuka kwa 80% zaidi ndani ya miaka mitatu iliyopita.

Ndio, kufa kwa Flash kwa kiasi kikubwa kumechangiwa na kuongezeka kwa matumizi ya smartphone. Apple walikataa kuruhusu Flash itumike kwenye iPhone miaka mingi iliyopita na kuwekeza nguvu zake katika matumizi ya HTML5, na pia Adobe waliacha kusupport Flash kwajili ya Android mwaka 2012. Now that a firm date is set, hopefully sites will start moving a bit quicker to remove their dependence on the aging plugin. Sasa tarehe ya mwisho imetangazwa na kampuni , Ni matumaini yangu tovuti zitaanza kuhama kwa haraka ili kuondoa utegemezi wao kwenye plugin hii ya kizee.
 Chanzo: Chromium Blog

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako