Sambaza:

Mwanzilishi wa Facebook na CEO Mark Zuckerberg amepata shahada ya heshima kutoka katika chuo kikuu cha Havard, Marekani.

Mark ambaye ni miongoni mwa matajiri wakubwa duniani kwa mujibu wa Forbes, aliwahi kusoma katika chuo hicho miaka 12 iliyopita. Baada ya Zuck kupatiwa heshima hiyo, kupitia mtandao wake wa Facebook alimuandikia ujumbe mama yake unaosomeka:

“Mom, I always told you I’d come back and get my degree.”

Miaka kadhaa iliyopita, bosi huyo aliwahi kukaririwa na gazeti la chuo hicho lijulikanalo kama “The Harvard Crimson” akisema hataweza kurudi tena chuoni hapo kusoma na badala yake atawekeza nguvu nyingi katika mtandao wake wa Facebook ambao ulikuwa unakuwa kwa kasi katika kipindi hicho.

SOMA NA HII:  Google Sasa Kuzuia Matangazo Kupitia Kisakuzi Kipya cha Chrome

Kwa sasa Mark mbali na kumiliki Facebook ambayo inautajiri wa $61.5 lakini pia anamiliki mitandao mingine kama Instagram na Whatsapp.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako