Nyingine

Mwanaume ukiwa maskini huwezi kuoa wake wengi Nigeria

Baada ya mmoja wa viongozi wakuu wa kiislamu nchini Nigeria kusema kuwa atatangaza sheria ambayo itawazuia wanaume kuoa zaidi ya mke mmoja kwa sababu tamaduni ya kuoa wake wengi imechangia kuwepo ugaidi kaskazini mwa nchi hiyo.

Sasa Spika wa bunge katika jimbo la Kano lililoko kaskazini mwa Nigeria, amesema kuwa umma utaombwa kutoa maoni yao kuhusu muswada wenye lengo la kuwazuia wanaume maskini kuoa zaidi ya mke mmoja.

Viongozi na wasomi wataombwa ushauri kuhusu ni nani haswa atatambuliwa kuwa maskini.

Pendekezo hilo lenye utata lilitolewa na Muhammad Sanusi II, ambaye ni Emir wa Kano, kuhakisha kuwa wanaume wana familia ambazo wanaweza kuzitunza.

Tangu aingie madarakani mwaka 2014, Emir Muhammad Sanusi II, amekuwa akitoa mapendekezo mengi yenye utata ambapo amepinga misimamo mingi ya kitamaduni.

SOMA NA HII:  Kuwa mkweli! Jina gani umetumia ku-save namba ya simu ya mama yako?

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.