Sambaza:

Mwanamuziki kutoka nchini Senegal na Marekani, Akon siku ya jumamosi alitangaza mpango wake wa kununua hisa asilimia 50 za kampuni ya huduma ya kupakua muziki wa Kiafrika Musik Bi, Kwa sasa kampuni hiyo inapambana kupata nafasi kubwa kwenye soko baada ya uzinduzi wake miezi 18 iliyopita.

Jukwaa la kwanza barani Afrika la kupakua muziki kisheria, Musik Bi ilizinduliwa nchini Senegal mnamo Februari 2016 ikiwa na lengo la kutangaza wasanii wa Afrika, kuwalipa vizuri, na kupambana na uharamia wa mtandaoni.

Akon, ambaye jina lake halisi ni Aliaune Badara Thiam, alitangaza huko Dakar kuwa atakuwa mmiliki mwenye hisa nyingi zaidi katika huduma hiyo, ameielezea Musik Bi kama “Jukwaa bora la siku zijazo”.

SOMA NA HII:  Watoto Uingereza kuanza kufundishwa zaidi kuhusu uelewa wa masuala ya digitali

“Siyo tu jukwaa kwajili ya Senegal bali ni kwajili ya Afrika,” aliongeza, japo alikataa kusema kiasi alicholipa kwajili ya manunuzi ya hisa hizo.

* WIMBO MPYA*

Anajulikana zaidi kwa nyimbo zake kama /Locked Up/ na /Smack That/, Miaka ya karibuni,Akon amewekeza muda wake kujitolea katika mradi wake wa “Lighting Africa solar energy initiative” na shughuli nyingine za kijamii.

Hivi karibuni ametambulisha wimbo wake mpya / Khalice /,ambao amefanya ushirikiano na mwanamuziki nyota kutoka Senegal Youssou Ndour, ambao ni exclusive kwenye Musik Bi.

Zaidi ya wanamuziki maarufu 200 wa kimataifa, pamoja na wasanii chipukizi, wanamuziki wa jazz na waimbaji wa nyimbo za dini, wamekubali kuweka nyimbo zao kwenye Musik Bi, ambapo watumiaji wanaweza kupakua kwa kutumia salio la Simu zao.

SOMA NA HII:  Marekani Inasema Korea ya Kaskazini Inahusika na Mashambulizi ya WannaCry

Mkurugenzi Mtendaji Moustapha Diop, ambaye kampuni yake ya Solid ilianzisha mradi huo, alisema migogoro inayoendelea kati ya mradi huo na makampuni ya simu juu ya mgawanyo wa mapato kati yao umezuia Musik Bi kuenea zaidi.

“Tuna malengo ya kusambaa Afrika nzima na kuwa jukwaa la usambazaji wa muziki Afrika, “Diop aliwaambia waandishi wa habari.

*TAMASHA LA MUZIKI*

“Faida inayotengenezwa na mitandao ya simu ni tatizo kwa sababu inaenda tofauti na maslahi ya wasanii na jukwaa kwa ujumla. Tutaendelea kujadiliana ili kupata mpango wenye faida kwa pande zote, “aliongeza.

Baada ya kampuni za simu kuchukua sehemu yao, wasanii wanachukua asilimia 60 ya Mapato yao kutoka kwenye huduma hiyo, wakati Musik Bi inachukua asilimia 40 iliyobaki.

SOMA NA HII:  SUA kuokoa asilimia 40 ya mazao yanayoharibiwa na panya shambani

Jukwaa pia linatarajia kupanuka na kuanzisha tamasha la muziki, televisheni Channel na huduma ya Streaming, Akon alisema.

Uharamia na kubadilisha tabia za watumiaji kumesababisha mauzo ya muziki kushuka Barani Afrika, huku kupakua kinyume cha sheria kukiwavutia zaidi watumiaji wa Afrika wanapotafuta muziki mtandaoni, utekelezaji wa hakimiliki bado ni dhaifu.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako