Sambaza:

Twitter imethibitisha kuwa imefungia zaidi ya accounts 377,000 ndani ya miezi sita ya mwisho wa mwaka 2016 kwa sababu ya kukuza ama kutangaza ugaidi.
Taarifa hii ilitolewa kwenye ripoti yao ya wazi ya mwaka 2016 ilitolewa tarehe 21 Machi, 2017 ambayo inachapisha data za maombi yanayo pokelewa na Twitter kutoka kwa serikali na vyombo vingine vya kisheria kuchunguza maudhui yaliyomo kwenye mtandao huo.

Ingawa ni akaunti 376,890 zilizosimamishwa na Twitter kwa kuchapisha vitu vinavyohusiana na ugaidi, asilimia mbili tu ni matokeo ya maombi ya serikali ya kuondoa taarifa hizo. Twitter wamesema asilimia 74% ya akaunti za watu wenye msimamo mkali zilipatikana kwa kutumia “internal, proprietary spam-fighting tools” ya mtandao huo.

Hii ni mara ya kwanza Twitter kuweka wazi jitihada zake za kupambana na vikundi vyenye msimamo mkali katika machapisho yake ya wazi tangu kampuni ilipoanza kutoa ripoti mwaka 2012.

Kwa ujumla, Twitter imesimamisha akaunti 636,248 kwa kuwa na msimamo mkali kati ya Agosti mwaka 2015 na Desemba 2016.

Sambaza:
SOMA NA HII:  SNORT mfumo wa bure wa Kugundua Kuvamiwa na Kuzuia

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako