Sambaza:

Cristiano Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza kufikisha magoli 100 kwenye UEFA kwa ngazi ya club baada ya kufunga magori mawili dhidi ya Bayern München.

Cristiano Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza kufikisha magoli 100 kwenye UEFA kwa ngazi ya club.

Mshambuliaji huyo kutoka Ureno alifungua account yake ya magori kwenye mechi ya Manchester United 3-0 dhidi ya Debrecen tarehe 9 Agosti 2005. Imepita miaka kumi na moja na miezi nane , usiku wa jana amefunga mala mbili Real Madrid ilivyotoka nyuma ya Bayern München na kufanikisha kupata ushindi.

Ronaldo alifikisha magoli 50 Aprili 2013 alipofunga magoli mawili dhidi ya Galatasaray. Alifikisha magoli hayo baada ya mechi 96 licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kufunga kwenye mechi 32 za kwanza kwenye mashindano ya Ulaya alipokuwa na Sporting CP na United.

Magori mengine 50 ameyafunga ndani ya mechi 47.

Wenye Magoli mengi kwenye UEFA kwa ngazi ya club (*ambao bado wanacheza)

100 – Cristiano Ronaldo* (mechi 143)

97 – Lionel Messi* (mechi 118)

76 – Raúl González (mechi 158)

70 – Filippo Inzaghi (mechi 114)

67 – Andriy Shevchenko (mechi 142)

62 – Ruud van Nistelrooy (mechi 92)

61 – Gerd Müller (mechi 69)

59 – Thierry Henry (mechi 140)

59 – Henrik Larsson (mechi 108)

56 – Zlatan Ibrahimović* (mechi 136)

SOMA NA HII:  Teknolojia 5 Maarufu kwenye Magari Kwa Sasa

54 – Eusébio (mechi 70)

53 – Alessandro Del Piero (mechi 129)

51 – Karim Benzema* (mechi 93)

50 – Didier Drogba (mechi 102)

50 – Klass-Jan Huntelaar* (mechi 82)


Sambaza:

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako