UTAFITI: Mvinyo mwekundu unaweza kutibu magonjwa haya makubwa


Utafiti mpya unasema mvinyo mwekundu ambao awali ulihusishwa na faida mbali mbali za kiafya, kuanzia kusaidia kupunguza kihatari za kupata magonjwa ya moyo na na kisukari una kemikali ambazo zinakabiliana na kuoza kwa meno na ugonjwa ufizi.

Katika utafitihuu uliochapishwa katika jarida la Kemikali za Kilimo na Chakula , wanasayansi walichunguza ikiwa kemikali ya mvinyo ya polyphenols inaweza pia kuwa nzuri kwa afya ya kinywa.

Watafiti walibaini kuwa mchanganyiko wa kemikali unaotengeneza kinywaji hicho, unaofahamika kama polyphenols, husaidia kumaliza kuwamaliza vimelea (bakteria) hatari kinywani.

Utafiti wa awali ulionnyesha kuwa faida za kiafya za polyphenols zilihusishwa na kuwa na uwezo wa kuulinda mwili dhidi ya vimelea hatari wanaoshambulia mwili.

Hata hivyo, utafiti wa hivi karibuni umeonyesha kuwa kemikali salama ya polyphenols inaweza kuboresha afya kwa kufanya kazi na “vimelea wazuri ” katika tumbo zetu.

Watafiti walilinganisha athari za aina mbili za kemikali ya polyphenols kutoka kwa mvinyo mwekundu dhidi ya mbegu ya zabibu na kiasi kidogo cha mvinyo mbadala kwenye bakteria wanaoganda kwenye ufizi na meno na kusababisha magonjwa ya kinywa, kuoza kwa meno naugonjwa wa ufizi.

Walibaini kuwa kemikali ya mvinyo na mvinyo kwa pamoja vilipunguza uwezo wa Bakteria wa kukaa kwenye seli, lakini kemikali zaa polyphenols – caffeic na p-coumaric acids – zilifanya kazi bora zaidi .

Mvinyo mwekundu una kiwango kikubwa cha kemikali za polyphenols, lakini pia zinaweza kupatikana katika machungwa, vinywaji na vyakula kama Kahawa, Chai ya majani chai mabichi, Chai ya kawaida ya maja, Maji ya machungwa na limao, maharagwe na Zabibu nyeusi.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA