Makala

Muziki Ni Zawadi Itumike Vyema

Hebu waza maisha bila muziki. Kuishi bila muziki unaotuliwaza, bila muziki wa kimahaba, bila nyimbo za kisasa zenye midundo yenye kuvutia, bila muziki wa kiokestra unaochochea hisia, na bila muziki mtamu usio na maneno. Huenda watu wengi wakahisi kwamba maisha bila muziki yanachosha na hayavutii.

Western Jazz Band

 

Kwa kweli, muziki hugusa hisia zetu kwa njia mbalimbali. Unatutuliza na kutusisimua, unatuchangamsha na kutuchochea. Unatufanya tuwe na shangwe nyingi na kutufanya tutokwe na machozi. Hata hivyo, kwa sababu muziki una uwezo wa kugusa mioyo yetu, una nguvu sana. Kwa nini muziki hutuchochea sana? Jibu ni rahisi: Muziki ni zawadi nzuri sana kutoka kwa Mungu. Kwa sababu hiyo, unapaswa kuthaminiwa, unapaswa kuwa wenye kujenga, na wote—wazee kwa vijana—wanapaswa kuufurahia.

Muziki umekuwapo tangu zamani. Kwa mfano, vitu vya kale vilivyochimbuliwa vinaonyesha kwamba karne nyingi kabla ya Wakati wetu wa Kawaida makabila ya Afrika yalipiga ngoma, baragumu, na kengele. Wachina wa kale walipiga kinanda cha aina fulani na zumari. Watu kutoka Misri, India, Israeli, na Mesopotamia walipiga kinubi.

Ni wazi kwamba ili mtu afurahie muziki uliopigwa katika nyakati hizo, ilimbidi apige au amsikilize mtu mwingine akipiga ala fulani ya muziki. Hata hivyo, tofauti na hilo, mamilioni ya watu leo wanaweza kupata muziki kwa urahisi sana. Leo, unaweza kurekodi au kupakua muziki wowote na kuusikiliza kupitia vifaa mbalimbali kutia ndani vile vinavyoweza kubebwa mfukoni. Uchunguzi mmoja uliofanywa katika nchi moja ya Magharibi mnamo 2009 ulionyesha kwamba vijana wenye umri wa kati ya miaka 8 na 18 hutumia zaidi ya saa 2 kila siku wakisikiliza muziki na habari nyingine zilizorekodiwa.

Mazoea hayo yanaonyesha kwa nini muziki pamoja na vifaa vya kisasa vya kurekodi na kusambaza muziki vinauzwa kwa wingi sana. Kwa kweli, uuzaji wa muziki pamoja na bidhaa za muziki umekuwa biashara kubwa sana. Lakini, je, umewahi kujiuliza ni mambo gani yanayohusika ili kutokeza muziki unaopendwa na kuuzwa kwa wingi?

SOMA NA HII:  Vidokezo 8 rahisi jinsi ya kukuza tukio lako kwenye LinkedIn

Muziki Kwenye Intaneti

KUPAKUA: Kwa kawaida watu hulipia faili ya muziki ambayo wanapakua, na hivyo inakuwa mali yao. Wengine hujiandikisha—mara nyingi wanaponunua simu au vifaa vingine vya kielektroniki—na hivyo wanaweza kupakua na kucheza muziki katika kipindi walichojiandikisha.

MUZIKI UNAOCHEZA MOJA KWA MOJA: Huu ni muziki uliorekodiwa na kuhifadhiwa katika vituo fulani vya Intaneti ambavyo mtu anaweza kusikiliza moja kwa moja bila kuupakua. Muziki huo hautozwi ingawa mtu anaweza kupakua kiasi fulani iwapo atajiandikisha kwenye kituo hicho.

Maendeleo Katika Kurekodi

Miaka ya 1880 – Gramafoni

Miaka ya 1890 – Kanda za sumaku

Miaka ya 1940 – Kanda ya kurekodiwa moja kwa moja

Miaka ya 1960 – Kanda za kaseti

Miaka ya 1980 – CD

Miaka ya 1990 – Faili za kielektroniki (MP3, AAC, WAV, n.k.)

Ni Nini Hufanya Kibao cha Muziki Kiuzwe Sana?

BIASHARA ya muziki inabadilika-badilika upesi na ina ushindani mkubwa. Mapendezi ya wasikilizaji hubadilika, miziki iliyopendwa inapitwa na wakati, na mbinu za kurekodi na kusambaza muziki zinatokea. Wadhamini “hutafuta muziki motomoto kila wakati”. Lakini si rahisi kufanya “muziki fulani” uuzwe kwa wingi. “Vijana wengi hutamani sana kuwa wasanii maarufu, . . . lakini si kazi rahisi kupata mkataba na kampuni ya kurekodi,”.

Kutunga Maneno ya Muziki

Wasanii hujaribu sana kutunga maneno yanayogusa hisia za watu—maneno ambayo hufanya watu watafakari kuhusu matumaini yao, matarajio, na hisia za ndani zaidi. Watu huimba hasa kuhusu nini? Ikiwa umejibu, mahaba, hilo ndilo jibu sahihi. Wasanii pia hujaribu kubuni mstari fulani wenye maneno yanayovutia sana ambayo yatanasa akili ya msikilizaji na kubaki akilini kwa muda mrefu.

SOMA NA HII:  Kuweka Mkeka "Kubeti" Njia ya Kutengeneza Pesa yenye Ugonjwa

Kisha, msanii hurekodi wimbo wake kwa mara ya kwanza, ili usikizwe na kampuni ya kurekodi. Ikiwa baada ya kusikiliza wimbo ule wasimamizi wa kampuni ya kurekodi wanaona kwamba wimbo huo utakuwa maarufu, huenda basi wakampa msanii huyo mkataba wa kurekodi . Lakini ikiwa hawana uhakika na msanii huyo (labda kwa sababu yeye si maarufu sana), wanaweza kununua wimbo huo na kumpa msanii mwingine maarufu zaidi.

Ndani ya Studio

Ili kusimamia kazi ya kurekodi , kwa kawaida kampuni za kurekodi humtafuta producer, au mtayarishaji, aliye na uzoefu. Yeye huamua mtindo ambao msanii atatumia na kuidhinisha rekodi ya mwisho ya wimbo huo. Yeye ndiye hutafuta na kusimamia studio ya kurekodia itakayotumiwa, anatafuta pia wapangaji wa muziki, wanakili wa muziki, wanamuziki, waimbaji wa ziada, mainjinia wa kurekodi, na vifaa vitakavyorekodi muziki wa hali ya juu ambao utawavutia wasikilizaji.

Nyimbo nyingi hurekodiwa hatua kwa hatua, mara nyingi kuanzia kwa kurekodi midundo ya ngoma, gitaa mbalimbali, na piano. Kisha, sauti za waimbaji wanaoongoza muziki hurekodiwa pamoja na zile zinazoambatana na ala za muziki, na madoido mengine ya pekee ya sauti huchanganywa ili kutokeza nakala ya awali ya wimbo uliorekodiwa kielektroniki .

Uuzaji

Ili muziki uwe maarufu na kuuzwa zaidi, mara nyingi makampuni ya kurekodi hutokeza video za muziki . Video hizo zenye urefu wa dakika tatu hadi tano huenda zikatokeza msisimuko kama ule wa tamasha ya muziki na pia kusaidia wasikilizaji kumwona na kumsikia msanii huyo. Pia video hizo zinaweza kuiletea kampuni ya kurekodi pesa nyingi sana.

SOMA NA HII:  Mfahamu Mwanzilishi Wa Kampuni ya Simu za Tecno - Tecno Mobile

Wasanii wa muziki huuza albamu nyingi zaidi katika maeneo wanakofanyia tamasha za muziki . Hivyo wao hutangaza kuhusu albamu zao mpya popote waendapo na wanapopanga kufanya tamasha za muziki. Pia wasanii wengi hufungua Tovuti  na kupachika baadhi ya nyimbo, picha, video, blogu za kibinafsi, habari kuhusu tamasha za muziki zijazo, kutia ndani viunganishi vinavyowaelekeza mashabiki kwenye vituo ambavyo wanaweza kutoa maoni yao, na pia wanawaelekeza kwenye vituo ambavyo muziki wao huuzwa.

Ni nani anayeamua ikiwa muziki utakuwa maarufu sana? Ni wewe—msikilizaji. Hivyo basi, ni nini hukuchochea uchague muziki fulani? Unapochagua muziki, je, wewe huvutiwa na mdundo tu au msanii, au wewe una viwango vinavyokuongoza? Haya ni maswali muhimu, kwa sababu muziki una nguvu na unaweza kutuathiri sana.

Je ni kwa jinsi gani unachagua muziki ? Na ikiwa wewe ni mzazi, unaweza kutimiza jukumu lako la kuwalinda watoto wako dhidi ya hatari za kiroho, kiakili, na kihisia zinazotokana na muziki wanao sikiliza?

Mabadiliko Katika Biashara ya Muziki

Intaneti, vyombo vya kurekodi muziki vya bei ya chini, pamoja na programu za kompyuta zimechangia sana mabadiliko katika biashara ya muziki. Siku hizi, wanamuziki wanaweza kurekodi muziki wa hali ya juu kwa ustadi sana wakiwa nyumbani na kuusambaza kote ulimwenguni. Kulingana na ripoti moja katika gazeti The Economist,

“wasanii maarufu sana walirekodi na kusambaza muziki bila kutumia kampuni yoyote ya kurekodi.”

Una maoni  gani kuhusu muziki na biashara ya muziki ?

Toa maoni yako.

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako