Intaneti

Muonekano wa tovuti ya Google katika simu janja umefanyiwa mabadiliko

Ukitafuta kitu kupitia tovuti maarufu ya Google siku ya leo bila shaka utaona kuna tofauti wa muonekano wa ukurasa wake.

Tofauti hiyo utakayoiona ni mabadiliko yaliyofanywa na Google wenyewe katika kuboresha ukurasa wake. Mabadiliko hayo yanapatikana kwa watumiaji wa simu janja wa mifumo endeshi ya Android na iOS.

Muonekano mpya katika sehemu kutafuta kitu kwenye Google.

Mabadiliko hayo utayaona katika boksi lake la msingi la utafutaji wa vitu mbalimbali ambapo sasa pembeni kumekuwa na mkunjo wa mviringo badala ya muonekano wa awali ambapo kulikuwa na ncha kali bila ya mviringo. Na kisha utaona mabadiliko mengine pale utakapo tafuta kitu na yatakapokuja majibu ya kile ulichotafuta utaona matokeo yote ya utafutaji yapo ndani ya mzunguko wa boksi maalum.

 Unayazungumziaje mabadiliko haya? Je, ni bora zaidi kuliko ilivyokuwa mwanzo, au Google imekosea kidogo? Hebu tuambie maoni yako!

SOMA NA HII:  Jinsi ya Kuepuka Makosa 5 Yanayofanywa na Wamiliki wa Website
Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako