Multiple WordPress Installation Kwa Kutumia Database Moja


Wakati mwingine kuinstall zaidi ya WordPress moja ni muhimu, lakini host yako inaweza kuwa na kikomo cha MySQL Database. Naam, suluhisho la tatizo hilo ni kuwa na installation nyingi za WordPress katika database moja.

Lazima uinstall WordPress manually ili mfumo huu uweze kufanya kazi. Programu nyingine kama Fantastic hazikuwezeshi kuchagua kiambishi awali (prefix).

Wakati wa installation kwenye config.php yako, unatakiwa kubadilisha kiambishi awali “wp_” ili kuruhusu multiple installation. Kwa hiyo inaweza kuwa wpbenix_ na inayofuata inaweza kuwa wpben_ unaweza kutumia prefix tofauti na kuzitumia kuunda installation nyingi kadri unavyohitaji.

Hivyo ndivyo unavyotakiwa kufanya. Hii pia ni kipimo cha usalama ambacho unaweza kuchukua hata kama huna haja ya kufanya multiple installation. Kwa kuwa na prefix, unafanya kazi ya hacker iwe ngumu zaidi ili kujua SQL Address kabla ya kuhack.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA