Sambaza:

KAMPUNI ya Multichoice Tanzania leo imetangaza huduma mpya kwa wateja wake baada ya kutangaza kufanya mapinduzi makubwa katika huduma yake ya DStv.

Kuanzia Novemba Mosi, mwaka huu wateja wa DStv wataanza kunufaika na punguzo la bei katika vifurushi vya Premium, Compact Plus, Compact, Family na Access.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Multchoice Tanzania, Ronald Shelukindo amesema kuwa DStv Premium imepokea punguzo la asilimia 16 kuanzia Novemba Mosi ambapo bei yake mpya itakuwa ni Sh 184,000. Pamoja na hayo pia kifurushi hicho kitakuwa na ongezeko la chaneli nane.

SOMA NA HII:  Airtel Money yatangaza gawio la bilioni 1.7 kwa wateja

Kifurushi cha DStv Compact Plus kimepokea punguzo la asilimia 17 na bei yake itakuwa ni 122,500. Chaneli hizo mpya zitarushwa na Vuzu, AMP, Lifetime, Discovery, Crime & Investigation, History na Africa Magic Showcase.

Compact Plus imeongeza pia chaneli za michezo zitakazoendeleza msisimko kwa wapenzi wa soka kupitia vipindi vya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ligi za Ulaya na Europa na zote zitapatikana kwenye chaneli ya Supersport 6 na 4,” alisema Shelukindo.

Aidha, kwa wapenzi wa filamu za kiafrika watafaidi kupitia Nollywood, wapenzi wa tamthilia za Kilatini, wataburidika na Telenovelas, filamu za Bollywood na sinema zitakazopatikana kwenye chaneli za ROK, Eva Plus na B4U.

SOMA NA HII:  Taarifa kutoka TANESCO kuhusu mfumo wa ununuzi wa umeme kwa njia ya LUKU

Kuhusu kifurushi cha Compact, bei yake mpya itakuwa ni 82, 250 ikiwa ni punguzo la 5%, kitakuwa na Ligi Kuu ya England, Premier na ile ya Ligi Kuu Hispania, La Liga lakini wateja wameongezewa chaneli za ITV Choice, TCM na Super Sport 4.

Kwenye kifurushi cha Dstv Family, bei mpya ni 42,900 na kimepokea ongezeko la chaneli tano za B4U Movies, Eva, Eva Plus, Supersport 4 na Fox.

Na kuhusu kifurushi cha Dstv Bomba, kuna ongezeko la chaneli tatu na bei yake mpya ni 19,950 kutoka 23,500,” aliongeza mkurugenzi huyo.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako