Ninaamini watu wengi kwa sasa wanamiliki laini za simu zaidi ya moja, lakini kuna laini moja ambayo hiyo ndio laini mama.

 Mtandao gani wa simu-mediahuru

Kila mtu ana uzoefu wake linapokuja swala la mtandao wa simu unaotoa huduma bora zaidi kwa maana ya uhakika wa upatikanaji na huduma zinazoendana na gharama zinazotozwa.

SOMA NA HII:  TAARIFA YA MKUTANO JUU YA MAPENDEKEZO YA VIWANGO VYA GHARAMA ZA MAINGILIANO YA MITANDAO YA SIMU NCHINI.

Kwa hapa Tanzania kwa sasa tuna mitandao mingi ya simu mingi ikiwa imejikita kwenye huduma ya sauti, huduma za kifedha na mingine kwenye huduma za data.

Mitandao hiyo ni TTCL, TIGO, VODACOM, AIRTEL, SMART, SMILE, ZANTEL na HALOTEL.

Kuna vigezo mbalimbali vya kuzingatia unapotoa maoni kuhusu mtandao wa simu unaoongoza kwa huduma bora. Zingatia vigezo hivi kutoa maoni yako:

  • Unaopatikana ukiwa mahali popote nchini (coverage)
  • Ubora na uwezo wa kuperuzi intaneti vizuri
  • Vifurushi vizuri na promotion nyingi
  • Huduma za kifedha (mobile financial services)
  • Huduma kwa wateja (Customer care & service)
  • Gharama nafuu kulingana na maisha yetu (gharama za malipo ya Sauti na Data)
  • Unaowajali na kuwathamini wateja wake

Pia unaweza kutoa maoni yako kwa kuongeza vigezo unavyovijua wewe au kulingana na matumizi yako ya kila siku.

Mtandao gani wa mawasiliano Tanzania unaongoza kwa kutoa huduma bora? Toa maoni yako.

 

Sambaza:

Written by Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako