Msanii Wema Sepetu kujiunga na CHADEMA rasmi, aungana na Mbowe mahakamani

Comment

Wema Sepetu akiwa Katikati ya Esther Bulaya na Mbowe hii leo.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilianio wa Chadema, Tumaini Makene amesema leo (Alhamisi) kuwa chama hicho kupitia Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe, baada ya kesi ya kikatiba namba 1 ya mwaka 2017 inayotarajiwa kuwasilishwa Mahakama Kuu leo, kitazungumza kwa umma kupitia waandishi wa habari kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo akiwemo Wema Sepetu

Leo, Wema na mama yake waliongozana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine wa chama hicho kwenye mahakama kuu jijini Dar es Salaam.

Ikumbukwe kwamba Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) na Mwanasheria mkuu wa CHADEMA, jana alijitokeza mahakamani kuwa wakili wa Wema na wenzake wawili. Msanii huyo aliyeshinda taji la Miss Tanzania mwaka 2006, alikuwa kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kabla ya kuhamia Chadema.

Chanzo:Jamiiforum

Up Next

Related Posts

Discussion about this post

error: Content is protected !!