Nyingine

Msanii Roma Mkatoliki na Moni Central Zone wavamiwa studio na kukamatwa

Mbunge wa Mikumi na staa Bongo Fleva Joseph Haule ‘Prof Jay’ ametoa taarifa kupitia account yake ya Instagram kuhusu kukamatwa kwa rapper Roma Mkatoliki pamoja na rapper Moni Central Zone katika studio za Tongwe Records na watu wasiojulikana jana usiku.

Profesa amedai watu hao wamemchukua pia kijana wa kazi, computer ya studio pamoja na TV.

Hii ni taarifa yake:

ROMA MKATOLIKI AMEKAMATWA USIKU HUU… Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za TONGWE RECORDS majira ya saa moja usiku na wamemchukua ROMA @roma2030 , MONI @moni_centrozone na kijana wa Kazi na pia wamechukua COMPUTER ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana.. Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi!!

SOMA NA HII:  Jinsi ya Kuepuka Makosa 5 Yanayofanywa na Wamiliki wa Website

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako