Nyingine

Movie 10 kutoka Afrika ambazo zitabadilisha jinsi unavyofikiri kuhusu umaskini

Unajua kuwa kila mwaka Nigeria “Nollywood” wanatoa movie nyingi kuliko Hollywood? Hapa tumekusogezea filamu na documentaries kumi kutoka barani Afrika ambazo unaweza kuziangalia!

1. Moolaadé (2004) | Senegal

Imeongozwa na baba wa filamu Afrika ,” Msenegali Ousmane Sembène, Moolaadé imegusia swala la ukeketaji. Hilo linaonyeshwa zaidi kwa Collé, mke wa pili katika familia ya wake wengi, ambaye anakataa kuruhusu binti yake kukeketwa . Pia alipinga wasichana watatu kutoka kijijini kwake kufanyiwa kitendo hicho. Filamu hii ilishinda tuzo ya ” Prize Un Certain Regard- Cannes mwaka 2004″.

2. The First Grader (2010) | UK / Kenya

Imeelezea hadithi ya kweli ya Kimani Maruge, mkulima wa Kenya ambaye aliojiunga na shule ya msingi akiwa na umri wa miaka 84 baada ya tangazo la serikali la elimu bure kwa shule za msingi mwaka 2003. National Geographic ilielezea tukio hilo kama “ushahidi wa ushindi wa nguvu wa mabadiliko ya elimu. ”

3. Neria (1993) | Zimbabwe

Miakaya 90 inaonekana kama kizazi cha dhahabu kwa “Zollywood” na Neria ni filamu iliyozungumziwa zaidi na ni filamu yenye hadhi ya juu kwa muda wote nchini humo. Inaonyesha masuala wanayomkabili mwanamke wa kijijini anapokuwa mjane, ikiwa ni pamoja na kupoteza mashamba yake na maisha yake. soundtrack imefanywa na shujaa wa Zimbabwe katika masuala ya utamaduni, Oliver Mtukudzi.

4. Big Men (2014) | USA / Ghana

Documentary hii inahusu ugunduzi wa mafuta katika pwani ya Ghana mwaka 2007 inajulikana kwa kuangalia utendaji kazi wa ndani wa makampuni makubwa ya mafuta. New York Times ilieleza documentary hii kama “cool and incisive snapshot of global capitalism at work.” Director Rachel Boynton imeisifia nchi ya Ghana kwa kupitisha “Extractive Industries Transparency Initiative” na kwa Wizara ya Fedha ya Ghana kutia nia ya kuchapisha uchambuzi wa kina wa risiti za mafuta na mgawanyo wake kila baada ya miezi sita.

5. Stealing Africa (2012) | Zambia

Katika miaka kumi iliyopita, makampuni ya kigeni yamechimba shaba yenye thamani ya zaidi ya $29 bilioni kutoka migodi ya shaba nchini Zambia, lakini bado ni moja ya nchi maskini zaidi duniani. documentary hii, ambayo inadai mapato mara kumi zaidi hupotea kutokana na mazoea ya kukwepa kodi inaangalia athari za vitendo hivyo kwa maendeleo ya nchi.

6. Stories of Our Lives (2014) | Kenya

Hadithi za Maisha yetu ni filamu ya Kenya, iliyotolewa mwaka 2014. Imetengenezwa na wanachama wa Nest Collective, kundi la sanaaa kutoka mjini Nairobi, filamu ni mkusanyiko wa filamu tano fupi  kuhusu hadithi ya kweli ya LGBT + life nchini Kenya.

7. Tsotsi (2005) | South Africa

Moja ya filamu zenye mafanikio zaidi kutoka nchini Afrika Kusini, Tsotsi (ambayo tafsiri yake ni “thug”) imeigizwa katika mji duni mjini Johannesburg. Inahusu kijana wa mtaani anayeiba gari na kugundua kuna mtoto. Filamu inaonyesha picha ya kijana aliyesahaulika kutoka kwenye jamii isiyokuwa na ukombozi . Tsotsi ilishinda Academy Award ya filamu bora yenye lugha ya kigeni mwaka 2005 na ilichaguliwa kwenye Golden Globe kama filamu bora yenye lugha ya kiingereza mwaka 2006.

8. Pirate Fishing (2014) | Sierra Leone

Thamani ya rasilimali za baharini kwa baadhi ya watu maskini zaidi duniani zimekuwa zikilengwa na viwanda vidogo vinavyojihusisha na shughuli haramu za uvuvi kwajili ya kupata vyakula vya baharini na kupeleka kwenye masoko ya Ulaya na Asia. Kwa kufanya kazi na Environmental Justice Foundation, uchunguzi huu wa Al Jazeera’s People & Power series ilitumia eneo la bahari ya Sierra Leone kufichua biashara ya uvuvi ya mamilioni ya dola inayofanyika kinyume cha sheria. Al Jazeera hivi karibuni walitengeneza “game” inayohusu documentary hiyo nakushauri tumia muda wako kuiangalia.

9. Virunga (2014) | UK / Democratic Republic of Congo

Virunga inalenga katika kuonyesha kazi za uhifadhi kwa askari wa ndani ya Virunga National Park na kuharibu shughuli za utafutaji wa mafuta ndani ya eneo la urithi wa dunia. Na ilichaguliwa kwenye tuzo za Academy kama Best Documentary Feature.

10. Beats of the Antonov (2014) | Sudan / South Africa

Documentary hii inahusu mgogoro wa Sudan-SRF katika eneo la Blue Nile na Milima ya Nuba, imelenga hasa kuonyesha umuhimu wa muziki, urithi na ubunifu asili katika kusaidia jamii zilizoathirika kwa malengo ya kujisaidia wenyewe kiutamaduni na kiroho katika kupambana na mgogoro unaoendelea.

Soma na hizi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close