AndroidSimu za Mkononi

Moto Z2 Force Edition: Simu mpya kutoka Motorola yenye teknolojia ya kuzuia kuvunjika kwa urahisi

Kama ilivyovyotarajiwa, Motorola wamepiga hatua nyingine leo hii kwa kutangaza rasmi mwanachama mpya wa smartphone kutoka kwenye kampuni hiyo: Moto Z2 Force Edition.

Simu hiyo ya smartphone inaingia sokoni ikiwa na mabadiliko makubwa. Mbali ya kuwa na vipengele vyenye ubora, pia ina kioo cha Quad HD AMOLED ambacho kina inchi 5.5 na ina teknolojia ya Motorola ShatterShield ili kuzuia kuvunjika kwa urahisi , hata kama simu imeanguka.

Maelezo mengine muhimu: Ni kuwa ina processor ya Qualcomm Snapdragon 835, RAM ya 4GB, na hifadhi(storage) ya ndani ya 64GB pia ina slot ya microSD ukihitaji uhifadhi(storage) zaidi. Moto Z2 Force Edition inatumia Android 7.1 Nougat, na Motorola wameahidi kutoa toleo la Android O katika siku zijazo (natumaini itakuwa karibuni). Pia ina betri ya 2730mAh, ambayo iko chini ya betri ya 3500mAh ambayo ilitumika kwenye Moto Z Force ya awali.

Nyuma, Moto Z2 Force Edition ina kamera mbili za megapixel 12. Moja ni Sensor ina rangi na nyingine ni monochrome, ambayo inaweza kutumika kuchukua picha za “black-and-white” badala ya kutegemea chujio(filter) kutengeneza aina hiyo ya picha.  Kuna kamera ya mbele ya megapixel 5 iliyounganishwa na flash ya mbele pia.

Moto Z2 Force Edition itapatikana katika rangi nyeupe, nyeusi na dhahabu inatarajiwa kuingia sokoni Agosti 10 kupitia AT & T, Verizon, Sprint, U.S. Cellular, na T-Mobile. Pia itauzwa kwenye tovuti ya Motorola na Best Buy. Inatarajiwa kuuzwa dola $299 (Tsh 666900) katika maeneo mengi, lakini inaonekana kama bei itaongezeka kwa wauzaji wa maeneo mengine. Kwa mfano, AT & T wanasema watauza $ 810.

SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Tecno W4 bei na Sifa zake

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako