IntanetiMagari

Moja ya nchi za Afrika ambazo haziunganishiki sasa kutoa Wi-Fi ya bure kwa wasafiri wa kigeni

Upatikanaji wa mtandao wa intaneti ni suala linaloendelea kuwa shida nchini Ethiopia, hata hivyo, shirika la mawasiliano la nchi hiyo limesema kuwa wateja wanaotumia “Bole International Airport” huko Addis Ababa watapata huduma ya bure ya mtandao wa intaneti.

Ethiopian Airlines

Benki ya Dunia inasema upatikanaji wa mtandao ni wa kiwango cha chini sana katika maeneo ya nchi hiyo, na watu 15% kati ya watu milioni 100 hivi sasa ndio wapo mtandaoni.

Kuzimwa kwa mtandao ni kawaida ndani ya nchi hiyo, hii imesababisha kikundi cha uhamasishaji chenye  makao yake makuu huko Marekani, Freedom House, kuiorodhesha Ethiopia kama nchi isiyo huru linapokuja swala la kutumia intaneti na uhuru wa habari.

SOMA NA HII:  Ifahamu ndege kubwa zaidi inayoweza kutua kwenye maji

Ethiopian Air inataka kutoa huduma ya bure ya intaneti kwenye kitovu chake kikuu katika mji mkuu wa Addis Ababa.

Hii ni sehemu ya jitihada za shirika hilo la ndege kuboresha huduma kwa wateja, kuboresha uzoefu wa abiria, na kufanya Bole International Airport kuwa bora barani Afrika.

Kwa kipindi kirefu, shirika la ndege la Ethiopia limekuwa linapambana kutekeleza nia yake ya kutawala anga la Afrika.

Mipango yake ya upanuzi pia imeongezeka kutokana na washindani wa kikanda kama Kenya Airways kuendelea kusuasua, kutokana na migomo ya wafanyakazi na matatizo ya kifedha.

Mnamo mwezi Agosti, Ethiopia pia ilitangaza kuwa ilikuwa katika mazungumzo ya kuchukua shirika la Arik Air, shirika kubwa la ndege nchini Nigeria.

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako