Kashfa ya Analytica, Mmiliki wa Facebook ameomba radhi kwa watumiaji wote


Mkurugenzi mkuu na mwanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerberg kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa kashfa ya Cambridge Analytica,amevunja ukimya na kudai kwamba wamefanya makosa na ameomba radhi kutokana na “kuvunja uaminifu” na weteja wake zaidi ya bilioni moja. Analytica inatuhumiwa kuingilia data za watumiaji million 50 wa mtandao wa Facebook.

Katika matamshi yake ya kwanza kuhusiana na matumizi mabaya ya taarifa binafsi za wateja zaidi ya milioni 50 kulikofanywa na kampuni ya Uingereza iliyokuwa na uhusiano na timu ya kampeni ya rais Donald Trump mwaka 2016, Zuckerberg amewaambia watumiaji wa Facebook kuwa taasisi yake “ilikuwa na wajibu wa kulinda taarifa.“ Amesema kitendo hicho kimewavunjia uaminifu. Hivyo kutokana na hali hiyo ameahidi kufanyika mabadiliko kadhaa ili kutoingiliwa na kuibwa kwa taarifa za watumiaji wake.

Ameahidi pia kuwa Facebook itachunguza kila programu iliyopata mwanya wa kupitia akaunti za wateja wake na kufanya uchunguzi wa kisayansi kwa kitu chochote kilichoonekana kina wasiwasi.

“Hii ilikuwa ni uvunjifu mkubwa wa matumizi ya taarifa binafsi na uaminifu, nawaomba msamaha kwa kile kilichotokea, wajibu wetu sasa ni kuhakikisha tukio hili halitokei tena.” -Zuckerberg

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA