Sambaza:

Meneja mkongwe hapa nchini, Said Fella amewajia juu watu wanaodai yeye ni miongoni mwa wanaochangia baadhi ya wasanii kutofanya vizuri kwenye muziki.

Mkubwa Fella amepinga vikali madai hayo wakati akiongea na 255 ya kipindi cha XXL cha Clouds FM.

“Mimi sina gazeti, sina redio, sina TV. Mimi mwenyewe nikija naomba kwa madj wanisaidie ngoma yangu ipigwe sasa inakuaje naua game?” amesema Fella.

“Vitu vingine vinavyoongelewa vinakuwa ni very poor, la msingi wanatakiwa wakaze na waje kuomba nimeanzaje kwa sababu wakae wakijua kwamba mimi ndio meneja wakwanza. Mimi nafundisha watu na wao waje niwafundishe lakini wakinilaumu wananilaumu bure,” ameongeza.

Sambaza:

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako