Habari za Teknolojia

Mitandao ya nchini Marekani yadukuliwa na ujumbe wa IS kuchapishwa

Mitandao ya Ohio yadukuliwa na ujumbe wa IS kuchapishwa

Mitandao kadha ya serikali katika jimbo la Ohio nchini Marekani ukiwemo wa Governor John Kasich imedukuliwa na ujumbe wa kuunga mkono kundi la Islamic State kuchapishwa.

Ujumbe huo ulisema , Donald Trump atawajibika kwa kila tone la damu linalomwagika kwenye nchi za kiislamu na kumalizia kusema “Naipenda Islamic State”.

Udukuzi huo ulifanywa na kundi linalojiita Team System DZ.

Ujumbe kwenye mtandao ulikuwa na ishara ya kiarabu na ulikuwa maandishi meusi na meupe ambayo hutumiwa kwenye bendera ya Islamic State.

Mtandao wa gavana wa jimbo la Ohio ulikuwa bado huajarekebishwa, ujumbe kwenye mtandao huu ulicheza wimbo wa kuitisha maombi ya kiislamu.

Mitandao ya Ohio yadukuliwa na ujumbe wa IS kuchapishwa
SOMA NA HII:  Hii ni amri ya serikali kwa wamiliki wote wa magazeti

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.