Mitandao ya kijamii kutumika kwenye kuomba visa Marekani


Serikali ya Marekani imeeleza kuwa itaanza kukusanya taarifa za historia ya mitandao ya kijamii ya karibu kwa kila mtu anayetaka kuomba visa ya kuingia nchini humo.

Pendekezo hilo lililotolewa na wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo, litawataka watu wote watakaokuwa wanaomba visa ya kuingia nchini Marekani kutoa taarifa zao za akaunti za Facebook na Twitter,

Taarifa hizo zitatumiwa kutambua na kuwachunguza watu wanaoomba viza za uhamiaji pamoja na zisizo za uhamiaji.

Waombaji wa visa pia wataulizwa kuhusu nambari za simu walizotumia katika kipindi cha miaka mitano, barua pepena historia yao ya kusafiri.

Takriban watu milioni 14.7 wataathiriwa na pendekezo hilo.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA