Nyingine

Mistari ya wimbo wa ‘Dear Mama’ iliyoandikwa kwa mkono na Tupac kuuzwa kwa $75k

Huku mashabiki wanafanya kila liwezekanalo ili kupata mali yoyote ile iliyoachwa na Tupac miaka 20 iliyopita, Mistari ya wimbo wa ” Dear Mama” iliyoandikwa kwa mkono wake sasa imewekwa kwa ajili ya kuuzwa. Kwa mujibu wa TMZ, MomentsInTime.com inauza mistari iliyoandikwa kwa mkono ya wimbo wa Tupac uliohit mwaka 1995 ‘Dear Mama.’

Kurasa tatu za barua ya upendo kwa mama yake Afeni Shakur zinauzwa kwa $ 25,000 kila mmoja, kwa jumla ni $ 75,000.

Inasemekana karatasi hiyo imetoka kwenye studio ambayo Tupac alirekodi wimbo huo na MomentsInTime.com wanasema waliinunu kwa private collector nchini Poland.

Hata hivyo, kwenye karatasi hiyo imeripotiwa kuna maandishi machache ya majina ya wasanii ambao huenda Tupac alitaka kushirikiana nao.

SOMA NA HII:  Je una bashiri "kubeti" ili kujikwamua na matatizo ya kimaisha ?

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako