Nyingine

Mikosi bado ya muandama Neymar atakiwa kujibu mashtaka ya ulaghai Madrid

Jaji mmoja katika jiji la Madrid ameamuru mchezaji nyota wa Brazil Neymar afikishwe kizimbani kujibu mashtaka ya ulaghai na ulaji rushwa alipokuwa anahamia Barcelona mwaka 2013.

Wazazi wa Neymar pamoja na rais wa klabu ya Barcelona wa wakati huo Josep Maria Bartomeu na mrithi wake Sandro Roselli pia wametajwa miongoni mwa washtakiwa.

Klabu ya Barca pamoja na Santos ya Brazil, alikotoka Neymar pia zinatakiwa kortini. Waendeshaji mashtaka wanadai klabu zote mbili zilidunisha makadirio ya thamani halisi ya mchezaji huyo ili kulaghai kampuni ya Brazil ambayo ingefaidika kutokana na uhamisho wake.

Kesi hiyo itasikilizwa mjini Madrid. Neymar ametakiwa kuweka dhamana ya zaidi ya dola milioni tatu unusu.

Kesi hiyo inatokana na malalamiko ya kundi la uwekezaji la Brazil DIS, ambalo lilimiliki asilimia 40 ya haki za uhamisho wa Neymar.

Waendesha mashtaka wanataka mchezaji huyo afungwe miaka miwili na kutozwa faini ya karibu pauni milioni 8. Hata kama mchezaji huyo atapatikana na hatia, itakuwa vigumu kufugwa jela. Chini ya mfumo wa sheria ya Uhispinia, kifungo cha chini ya miaka miwili kwa kawaida hutupiliwa mbali.

Waendesha mashtaka pia wanataka kuwatoza faini £7.2m Barcelona na £5.6m kwa klabu ya Santos.

Soma na hizi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close