Miezi 9 Baada ya kushinda EPL, Leicester City imefanya maamuzi magumu kwa kocha wao Claudio Ranieri

Bingwa mtetezi wa ligi kuu England Leicester City imemtimua Kocha wake muitaliano Claudio Ranieri, ikiwa ni miezi...

1 0
1 0

Bingwa mtetezi wa ligi kuu England Leicester City imemtimua Kocha wake muitaliano Claudio Ranieri, ikiwa ni miezi tisa baada ya kuiwezesha kupata ubingwa wa Ligi kuu.

Leicester msimu huu imekuwa ikiyumba iko katika nafasi ya 17, na ikipoteza alama moja tu itakuwa kwenye mstari wa kushuka daraja.

Kutimuliwa kwa kocha huyo kumekuja saa 24 baada ya kichapo cha magoli 2-1 walichopata kutoka kwa FC Seville.

Leicester City msimu uliopita ilitwaa ubingwa kwa zaidi ya alama 10 mbele, lakini msimu huu, mpaka sasa wamecheza michezo 25 ya ligi na kushinda mitano pekee, na imesalia michezo 13 ligi kuisha.

In this article

Join the Conversation